Mapambano yanaendelea
Huyu pichani ni Ayatollah Mpya wa wa muda wa Iran 👉Iran imepata Ayatollah mpya wa Muda
Ayatollah Alireza Arafi, ambaye alikuwa kiongozi wa zamani wa shule za kidini/seminari za Iran na mkuu wa Qom Friday, ameteuliwa na Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu takriban 88 kuiongoza Iran
Kwa sasa Ayatollah Alireza Arafi ndio Kiongozi Mkuu wa kiroho na Serikali wa Muda mpaka Atakapo Thibitishwa au kuchaguliwa mwingine na baraza la wanazuoni wa Kiislamu wapatao 88.
Fahamu kua Ayatollah ni mfumo sio mtu.
Ayatollah Alireza Arafi ni mwanazuoni wa Kiislamu wa na kiongozi wa kidini na kisiasa kutoka Iran ambaye amekuwa mmoja wa makasisi wenye ushawishi mkubwa ndani ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
Alizaliwa mwaka👉1959, Meybod, Iran
Hizi ni Nafasi muhimu alizowahi kushika
👉Mwanachama wa Baraza la Walinzi
👉Mwanachama wa Baraza la Wataalam
👉Mkuu wa seminari za kidini Iran
👉Imam wa sala ya Ijumaa mjini Qom
👉Mkuu wa Chuo cha kimataifa cha Al-Mustafa
Ayatollah Arafi alipanda ngazi za uongozi kupitia uteuzi wa nafasi za kimkakati ndani ya taasisi za kidini na kisiasa. Ushawishi wake uliongezeka sana baada ya kuteuliwa kuongoza mtandao mkubwa wa seminari za Iran, ambapo alisimamia mafunzo ya kizazi kijacho cha wanazuoni wa dini.
Alijulikana pia kwa kushiriki katika diplomasia ya kidini 👉mfano mwaka 2024 alifanya ziara Moscow kuzungumzia ushirikiano wa Iran na Urusi, jambo lililotafsiriwa kama ishara ya kupewa majukumu makubwa zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya kimataifa Arafi ameteuliwa kuwa mjumbe wa kisheria katika Baraza la Uongozi la muda la Iran.
Baraza hili lina jukumu la kutekeleza majukumu ya Kiongozi Mkuu wa nchi kwa muda hadi Baraza la Wataalam litakapochagua kiongozi mpya.
Baraza hilo lina wanachama watatu👉 Rais wa Iran, Mkuu wa Mahakama, na mwanachuoni mmoja ambaye sasa ni Arafi.
Si yeye pekee ndiye Kiongozi Mkuu kwa sasa bali ni sehemu ya uongozi wa muda wa pamoja.
Anasisitiza kulinda mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu dhidi ya kile anachokiita njama za kimataifa.
Ameelezea msimamo mkali dhidi ya ukana Mungu na pia anakosoa baadhi ya mifumo ya kidini ya ndani.
Kwa ufupi 👉Ayatollah Alireza Arafi si mtu wa kawaida bali ni sehemu ya safu ya juu kabisa ya viongozi wa kidini na kisiasa Iran. Kwa sasa amepewa jukumu la juu la mpito katika uongozi wa taifa wakati mchakato wa kumpata Kiongozi Mkuu mpya ukiendelea.
Endelea kua Nami Mchambuzi wako Profesa Chotara Mweusi Sultan Bingwa Wa uchambuzi kutoka Viunga vya Sharif Shamba Ilala Dar Es Salam.

Comments