MAJESHI YA URUSI CHINA NA IRANI YAANZA MAZOEZI YA PAMOJA DHIDI YA MAREKANI

Mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Russia, China na Iran karibu na Strait of Hormuz yana ujumbe wa kimkakati zaidi kuliko kijeshi pekee.  Siku za Hivi Karibuni Mataifa haya yamekua yakishirikiana sana katika mazoezi ya moja kwa moja.

Fuatana nami Mchambuzi wako Profesa Chotara Mweusi Sultan.

Huu ni Ujumbe kwa NATO na Marekani pamoja na Mshirika wao Israel mazoezi haya yanaashiria mambo makuu matatu.

👉Onyo la kisaikolojia, Ni ishara kwamba mataifa hayo yanaweza kushirikiana kijeshi ikiwa mgogoro mkubwa utatokea.

👉Ushirikiano unaokua, Inaonesha ushirikiano kati ya wapinzani wakuu wa Magharibi unaongezeka, hasa katika nyanja za ulinzi.

👉Kuzuia presha za kijeshi Yani Ni njia ya kuonesha kwamba mashinikizo ya kijeshi au vikwazo haviwezi kuitenga Iran kirahisi na wapo tayari kwa lolote iwapo litatokea.

Huu ni Ujumbe kwa Marekani Yani United States, mazoezi haya ni ishara ya kukaribisha vita Yanakusudia kuonesha kuwa shambulio lolote dhidi ya Iran linaweza kusababisha athari pana zaidi kuliko ilivyotarajiwa.

Marekani imezoea kuwa na uwepo mkubwa wa kijeshi Ghuba ya Uajemi Bila upinzani, hivo basi mazoezi haya yanaonesha kuna nguvu mbadala zinazoweza kupunguza ukiritimba Wa Marekani pia zipo na ziko tayari kwa lolote.

Ujumbe huu pia unakwenda moja kwa moja kwa Israel, Onyo la kimkakati linalo ashiria kwamba hatua za kijeshi dhidi ya Iran zinaweza kuhusisha wadau wengine wakubwa Kuliko wanavyo fikiria.

Hata kama mazoezi si muungano rasmi wa kijeshi, yanaongeza hatari ya mgogoro kupanuka iwapo vita vitaanza.

Ni muhimu kutofautisha kati ya ishara ya nguvu na muungano wa vita halisi

Mazoezi ya pamoja hayamaanishi moja kwa moja kuwa mataifa hayo yataingia vitani pamoja.

Mara nyingi mazoezi ya aina hii hutumika kama diplomasia ya kijeshi, si maandalizi ya vita.

Mataifa makubwa mara nyingi hufanya mazoezi ya pamoja ili kuboresha uratibu, si lazima kwa lengo la kushambulia mtu.

Mazoezi hayo ni zaidi ya ujumbe wa kisiasa kuliko maandalizi ya vita. Yanataka kuonesha mshikamano, uwezo wa ushirikiano.

Hata hivyo, hayaoneshi moja kwa moja kuwa kuna muungano rasmi wa vita dhidi ya upande wowote ni sehemu ya mchezo mkubwa wa nguvu unaoendelea duniani kama Mnavyo fahamu kwa sasa Iran ndio Super power ya mashariki ya kati kwahiyo inaungana na Wakubwa wenzake katika mazoezi ya Ukubwa wao.

Nihitimishe kwa kusema 👇 

Baki na Mimi kwa Mengi zaidi yanayo jiri Duniani 

By Professor Chotara Mweusi Sultan kutoka viunga vya 👇 
👉Sharif shamba 
👉Ilala Dar es salaam 
👉Tanzania 

Bingwa la uchambuzi wa maswala ya kijamii, Uchumi na Siasa za Dunia Yetu.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

ASANTE GWIJI YAYA TOURE KWA KUPASUA UKWELI UKWELI KUPENDELEWA KWA MOROCCO

CONFIRMED HAWA NDIO WACHEZAJI WETU 12 WA KIGENI 🦾

KILA MWANAMKE ANAPASWA KUFAHAMU HII...

RAIS WA SENEGAL AWAPATIA ZAWADI NONO WACHEZAJI WALIOFANIKISHA UBINGWA WA AFCON 2025

NYOMI YA WASENEGALI WAKISHANGILIA UBINGWA WA AFCON 2025

TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

MAMBO MADOGO YANAYOVUTIA KWA MPENZI WAKO