DKT. MAJULE AKABIDHIWA CHETI CHA SHUKRANI UWT DODOMA KUFANIKISHA USHINDI WA CCM 2025



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) akitoa cheti kwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Dkt. Neema Majule ikiwa ni miongoni mwa mikoa iliyoshiriki kufanya kampeni na kutafuta kura za kishindo kwa Mgombea wa Nafasi ya Urais kwa Tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wabunge pamoja na Madiwani katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 29, 2025.

Aidha, Chatanda alitoa vyeti vya Shukrani pia kwa Viongozi wa UWT kwa kila Mkoa Nchini, pamoja na Maafisa Tehama waliohakikisha kila taarifa za Uchaguzi zinawekwa kwenye mfumo mmoja na kupata takwimu sahihi kwa kile kilichofanyika katika kusaka ushindi wa kishindo kwa CCM.

Hayo yamejiri Februari 14, 2026 wakati wa kikao cha Baraza Kuu la UWT kilichoketi katika ukumbi wa NEC jijini Dodoma.

Dkt. Majule akipokea cheti hicho kutoa kwa Mwenyekiti wa UWT Taifa, Chatanda.


Dkt. Majule akifurahia na viongozi wenzie kupata cheti hicho.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203

 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

NI MAKOSA WANAFUNZI KUFIKA SHULE SAA 1:15 ASUBUHI

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

VIONGOZI NA WATENDAJI WA MATAWI UVCCM PANGANI WANOLEWA

NMB YAWAUNGANISHA WANANCHI NA HUDUMA, FURSA ZANZIBAR