KWA NINI MAASKOFU JANA KWENYE IBADA YA KUMUAGA PENGO WALIVAA MAVAZI MEUPE WAKATI NI MSIBA..?

Na

     Cosmasy William Choga 

Jibu ni kwamba mara nyingi hutumika rangi nyeupe badala ya nyeusi au zambarau kwa sababu  nyeupe ni rangi ya Ufufuko na tumaini la uzima wa milele.

Kwenye  teolojia ya Kikatoliki, Misa ya mazishi si tu maombolezo, bali ni  ibada ya matumaini kwamba marehemu anashiriki katika ushindi wa Kristo dhidi ya kifo. Hivyo, kwa viongozi wa Kanisa waliolitumikia kwa hadhi ya juu kama Kardinali huchukuliwa  zaidi kwenye fumbo la Pasaka kuliko huzuni.

Kardinali ni mshiriki wa Baraza la Makardinali chini ya Papa, na mazishi yake yanafanyika kwa heshima ya kiutume. Nyeupe inaonyesha heshima ya liturujia na hadhi ya ofisi aliyokua nayo, pamoja na ishara ya ushindi wa imani aliyouhubiri.

Tokea marekebisho ya liturujia baada ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatikano, Kanisa liliruhusu matumizi ya rangi nyeupe katika Misa za wafu ili kuonyesha zaidi matumaini ya Kikristo kuliko alama ya maombolezo mazito ya kale.

Lakini ikumbukwe kuwa si lazima iwe nyeupe kila mahali. Rangi inayoruhusiwa kwa mazishi kwa Romani Katoliki ni  Nyeupe (tumaini la ufufuko),Zambarau (toba na sala kwa marehemu) na Nyeusi (maombolezo ya jadi, hutumika mara chache leo).

Kwa vazi jeupe katika  mazishi ya Kardinali yana ujumbe wa kiimani, kifo kinaangaliwa kwa mwanga wa Pasaka, si kama mwisho bali kama mpito kwenda uzima wa milele. 

Kama kuna nyongeza unaweza jazia hapo kupitia uwanja wa maoni.

Deus omnes in fide Ecclesiae Catholicae benedicat.🤲🤲🤲🤲🤲🤲🤲🤲



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

KILA MWANAMKE ANAPASWA KUFAHAMU HII...

MBUNGE DKT. MAJULE ATOA MSAADA WA VYAKULA, VYANDARUA 100 SHULE YA VIZIWI DODOMA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

MAMBO MADOGO YANAYOVUTIA KWA MPENZI WAKO

DKT. MAJULE AKABIDHIWA CHETI CHA SHUKRANI UWT DODOMA KUFANIKISHA USHINDI WA CCM 2025

MAJESHI YA URUSI CHINA NA IRANI YAANZA MAZOEZI YA PAMOJA DHIDI YA MAREKANI

PUNGUZA STRESS....