Mbunge wa Viti Maalumu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Dodoma, Dkt. Neema Majule (katikati) akikabidhi msaada wa vyandarua 100 kwa Mkuu wa Shule ya Viziwi Dodoma,Awadhi Mbogo katika tukio lililofanyika Februari 21, 2026 katika shule hiyo iliyopo Kisasa jijini Dodoma.
Katika tukio hilo, Dkt. Majule ambaye yupo mstari wa mbele kujitotea kwa hali na mali katika masuala ya kijamii na hasa wenye uhitaji maalumu, alitoa pia misaada ya vyakula (mchele, unga, mafuta, sukari) na vinywaji pamoja na vifaa vya usafi.
Kabla ya makabidhiano ya msaada huo, Dkt. Majule alipata wasaa wa kutembelea na kujionea jinsi wanafunzi wanavyopata mafunzo kwa njia ya vitendo ikiwemo ushonaji, kompyuta, ufundi umeme na uselemala lakini pia mchezo wa pooltable.
Mkuu wa shule hiyo, Mbogo alitoa shukrani kwa kitendo cha mbunge huyo kuamua kutoa msaada huo mkubwa kwa shule hiyo na kwa aendelee na moyo huo wa kujitolea na kutoa wito kwa wananchi wengine kuiga mfano huo.
Shule hiyo ambayo ni ya serikali, chini ya Manispaa ya Dodoma inasimamiwa pia kwa msaada wa Robin Donker Sgoed ambaye ni Mwasisi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Environmental Oriented and Training Support.
Akigawa vyandarua hivyo kwa wanafunzi.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA- 0754264203



Comments