UWT YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI YA RUFAA DODOMA

JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake ya Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), imetoa msaada wa vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni moja ya shamrashamra ya  kuadhimisha miaka 49 ya kuzaliwa kwa  chama hicho.

Akitoa msaada huo kwa niaba ya Mwenyekiti wa UWT, Mary Chatanda, Katibu Mkuu wa UWT, Suzani Kunambi amesema kuwa vifaa hivyo vyenye thamani ya sh. mil. 20 ni maalumu kwa ajili ya Wodi za wajawazito na watoto Njiti.

Ametaja vifaa hivyo vilivyopokelewa na Mganga Mfawidhi msaidizi wa hospitali hiyo, Sara Ludovick kuwa ni; vitanda, mashine za kuleta joto kwa watoto Njiti, sabuni, mafuta na khanga.

Katibu Mkuu na wajumbe alioambatana nao walipata wasaa wa kuwatembelea wodi za wazazi na watoto njiti na kuwagapatia wazazi baadhi ya vifaa hivyo pamoja na vitu hivyo vingine.

Kunambi ambaye aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, baadhi ya viongozi wa UWT Taifa, UWT Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Dodoma walipanda miti kwenye viunga vya hospitali hiyo.

Kunambi akikabidhi mashine ya kuwapatia joto watoto Njiti.

Akikabidhi khanga.

Akikabidhi sabuni za unga.

Kunambi akikabidhi sabuni kwa mmoja wa wazazi katika wodi ya wazazi.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Neema Majule akimshika mmoja wa watoto waliozaliwa katika hospitali hiyo.
Kunambi akiangalia jinsi watoto njiti wanavyolelewa katikawodi maalumu.
Kunambi akimwangalia mmoja wa watoto




 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

KILA MWANAMKE ANAPASWA KUFAHAMU HII...

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

MBUNGE DKT. MAJULE ATOA MSAADA WA VYAKULA, VYANDARUA 100 SHULE YA VIZIWI DODOMA

MAMBO MADOGO YANAYOVUTIA KWA MPENZI WAKO

DKT. MAJULE AKABIDHIWA CHETI CHA SHUKRANI UWT DODOMA KUFANIKISHA USHINDI WA CCM 2025

30 TANZANIAN PROJECTS IN THE NEXT 10 YEARS