Taratibu za kikatiba za serikali ya Kiislam ya Iran, taratibu za kumchagua mrithi wa kiongozi mkuu ndio jukumu la kwanza la baraza la wataalam. Chombo kimepewa jukumu la kumuangalia kiongozi aliopo na kuchagua mrithi wake kulingana na dini na wasifu/muelekeo wake kisiasa.
Tayari kuna watu watano wanaotazamwa kumrithi kiongozi wa sasa endapo atafariki au kushindwa kuendelea na majukumu yake.
1. Mojtaba Khamenei, huyu ni kijana wa pili wa kiongozi wa sasa, anapewa nafasi kubwa kumrithi Baba yake kutokana na ukaribu walionao pamoja na ushawishi wake ndani ya jeshi la Iran 🇮🇷. Ana fikra na misimamo kama ya baba yake.
2. Alireza Arafi, kiongozi wa dini mwenye cheo cha juu na kiongozi wa Iran Seminaries pia makamu mwenyekiti wa baraza la wataalam (wafanya maamuzi). Anaaminika kuwa muendelezo wa Ally Khamenei. Anaaminiwa zaidi na viongozi wa dini na wanasiasa.
3. Gholan Hussein, Kiongozi wa juu wa mahakama na jasusi mstaafu. Ana maelewano makubwa na vyombo vya ulinzi pia ni kipenzi cha wafuasi wa itikadi za Ally Khamenei.
4. Ali Larijani, kamanda wa jeshi mstaafu, mwanasiasa mkongwe na anayefahamika mtu anaye meneji utawala pale zinapotokea changamoto.
5. Mohsen Qomi, Mshauri wa juu wa kiongozi wa sasa. Mtu wa ndani anayeaminika zaidi na mwenye uwezo wa kuendeleza utawala uliopo.
Kauli mbiu ya Iran ni "Khamenei-ism without Khamenei" yaani itikadi, sera na mitazamo ya Khamenei hata asipokuwepo Khamenei.

Comments