TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA

Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) limetangaza orodha mpya ya timu bora duniani kwa mwaka 2026, ambapo Tanzania imepanda katika Orodha hiyo, ikiendelea kuimarisha hadhi yake katika soka la kimataifa. Orodha hiyo imetokana kwa kiasi kikubwa na matokeo ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025.


Morocco wameongoza kwa kupanda kwa kiwango kikubwa zaidi barani Afrika, wakifikia nafasi ya nane duniani licha ya kupoteza fainali ya AFCON dhidi ya Senegal. Senegal nao wamepanda hadi nafasi ya 12 kutoka nafasi ya 17 waliyokuwa nayo mwaka 2024. Morocco mwaka jana walikuwa nafasi ya 11, huku nafasi yao bora kuwahi kushika ikiwa ya 10 mwaka 1998.

Kwa timu nyingine za Afrika, Nigeria waliomaliza nafasi ya tatu AFCON wameorodheshwa nafasi ya 26, Misri wako nafasi ya 31, Cameroon nafasi ya 45, huku Gabon wakishuka hadi nafasi ya 86 baada ya kutolewa mapema. Katika orodha ya jumla, Hispania wanaongoza duniani wakifuatiwa na Argentina, Ufaransa, England na Brazil, huku Ureno na Uholanzi wakishika nafasi ya sita na saba mtawalia.

Afrika Mashariki

Taifa stars ya Tanzania imepanda kwa nafasi mbili na kufikia nafasi ya 110 baada ya kushamiri kwenye dimba la Afcon wakitoka hatua ya raundi ya16 mara ya kwanza kwenye historia.

Uganda nao wameshuka kwa nafasi tatu baada ya kuboronga kwenye AFCON,wameorodheshwa nafasi ya 88 baada ya kushindwa kushinda hata mechi moja kwenye michuano hiyo.

Harambee star s wa Kenya wamedorora kwenye orodha hiyo baada ya kukosa kushiriki Afcon kwa mara ya tatu,wako nafasi ya 113.


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

BODABODA ALIPWA PIKIPIKI BAADA KUSAFIRI KWA BODA KWA SAA 10 MBEYA HADI DAR

ASANTE GWIJI YAYA TOURE KWA KUPASUA UKWELI UKWELI KUPENDELEWA KWA MOROCCO

CONFIRMED HAWA NDIO WACHEZAJI WETU 12 WA KIGENI 🦾

RAIS WA SENEGAL AWAPATIA ZAWADI NONO WACHEZAJI WALIOFANIKISHA UBINGWA WA AFCON 2025

NYOMI YA WASENEGALI WAKISHANGILIA UBINGWA WA AFCON 2025

Wasifu wa Kizza Besigye

CCM YAMJIBU BUTIKU CHADEMA KUFUNGIWA

SPIKA ZUNGU KUHUDHURIA MKUTANO WA 28 WA MASPIKA WA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA IND