Serikali ina mpango wa kuanzisha huduma za mabasi maalumu yaendayo haraka kwa ajili ya wanafunzi, hususan katika nyakati za asubuhi na jioni, ili kuhakikisha wanafunzi wanafika shuleni na kurejea majumbani kwa usalama na kwa wakati.
Mpango huo umeelezwa na Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma leo, alipokuwa akimjibu malalamiko ya mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani ya Dar es Salaam jinsi wanafunzi wanavyonyanyaswa na makondakta WA daladala kwa kukataa kuwapakia.
Katika kukabiliana na changamoto za usafiri wa abiria wakiwemo wanafunzi, Katika kuboresha usafiri wa wanafunzi mijini, serikali imeweka mipango na mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na:
kutenga mabehewa maalumu kwa ajili ya wanafunzi kwenye treni za mijini (Dar es Salaam), hatua inayolenga kupunguza msongamano, kuongeza usalama na kutoa unafuu wa usafiri kwa wanafunzi wanaotumia treni za mijini;
kurasimisha na kusimamia utozaji wa nauli maalumu ya Shilingi 200 kwa wanafunzi katika mabasi yaendayo haraka na daladala, kwa mujibu wa taratibu na kanuni zilizowekwa. Hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata huduma hizi kwa gharama nafuu; na
Kutekeleza Sheria na Kanuni za Kuthibitisha Madereva na Kusajili Wahudumu (Makondakta) wa vyombo vya usafiri wa Umma – Mabasi na Treni
Hatua zote hizi zinalenga kutekeleza malengo ya Serikali ya kuboresha huduma za kijamii, hususan huduma za wanafunzi katika vyombo vya usafiri, ili kuwawezesha kupata elimu katika mazingira r
Comments