Marekani imeikamata meli ya mafuta ya Urusi iliyokuwa ikitokea nchini Venezuela, ukamataji huo umefanyika pamoja na Urusi awali kuitaka Marekani isifanye ukamataji huo, shirika la habari la Reuters limeripoti jioni hii
Meli hiyo ya mafuta ya Urusi ilikua inasindikizwa na nyambizi ya kivita ya Urusi katika bahari ya Atlantiki, jeshi la Marekani limeikamata na kusema ilikua inajaribu kukwepa vikwazo vilivyowekwa na Marekani kwa meli zote kutoka Venezuela
Ukamataji huu ni mvutano wa moja kwa moja kati ya wababe wa dunia Urusi na Marekani, Urusi ilitoa tamko rasmi kuitaka Marekani isiikamate meli yao ila Marekani kapuuza tamko hilo
Jana rais wa Marekani alisema Marekani ina jeshi imara na lenye vifaa vya kisasa na silaha hatari kuliko mataifa yote ulimwenguni na hakuna taifa lolote duniani linaloikaribia Marekani hata kidogo kwa teknolojia na nguvu za kijeshi
Je Urusi itajibu nini?... See more

Comments