Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, amewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi na kupokelewa na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Anisa Mbega Januari 14, 2026 Jijini New Delhi nchini India.
Mhe. Spika amefika nchini India kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 28 wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola.
Mkutano huo wa siku tatu (3) unategemewa kufunguliwa leo Januari 15, 2026 na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi.


Comments