DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

 Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian akilakiwa kwa bashasha na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Mkoa huo, Dkt. Neema Majule alipowasili katika Shule ya Rhema eneo la Mlimwa kwa ajili ya kukabidhi msaada wa cherehani 120 kwa wanawake wa Dodoma Mei 27, 2026.

Balozi huyo pamoja na ujumbe wake  wameonesha kufurahishwa na mapokezi hayo yaliyohanikizwa na wanafunzi, walimu na baadhi ya wanawake wa mkoa huo waliokuwa wakipeperusha bendera za Taifa za China na Tanzania pamoja na ngoma ya asili ya kabila la wagogo iliyokuwa ikichezwa na wanafunzi wa shule hiyo.

Balozi Mingjian na Dkt. Majule wametiliana saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano baina ya wanawake wa China na wanawake wa Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Balozi Mingjian ameusifu ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya China na Tanzania.












IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA

UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MSALATO DODOMA KUANZA KUTUMIKA SEPTEMBA 2026

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Wasifu wa Kizza Besigye