*UCHAMBUZI: "UMASIKINI WA MWANAHABARI NI MTEGO WA MWANASIASA"*

*1. Kitendawili cha Uhuru na Tumbo (Economic Censorship)*

Waziri Makonda yuko sahihi kusema kuwa "Uhuru ni mgumu ukiwa masikini." Kitalamu, mwandishi anayewaza kodi ya nyumba na mlo wa watoto hawezi kuwa na utulivu wa kufanya *Investigative Journalism (IJ)* dhidi ya kigogo aliyempa shilingi 50,000 ya "nauli" asubuhi. Lakini swali la kitalamu kwa Waziri ni: *Nani amesababisha umasikini huu?* Umasikini wa vyombo vya habari nchini umetokana na serikali kuhodhi soko la matangazo na kutumia sheria kandamizi zinazofanya wenye vyombo waogope kuandika habari "ngumu" ili wasinyimwe matangazo au kufungiwa.

*2. Kifo cha Habari za Uchunguzi (The Death of Investigative Journalism)*

Mfano nzuri ni ripoti za CAG. Tunaona mabilioni yakipotea, lakini hakuna mwandishi anayeingia "chimbo." Sababu ni mbili:

* *Ukata:* Kitalamu, habari ya uchunguzi ni gharama (Fuel, informants, protection, equipment).

* *Woga:* Leo hii mwandishi akifichua ukwasi wa kiongozi, badala ya kiongozi kuchunguzwa, mwandishi ndiye anaanza kusakwa kwa "uchochezi" au "cybercrimes." Hali hii inawafanya waandishi wawe *"Public Relations Officers"* (Maafisa Habari) wa serikali badala ya kuwa mbwa wa mlinzi (*Watchdogs*).

*3. Magazeti na Kuporomoka kwa Soko*

Ni kweli magazeti sasa hayachapwi kwa wingi (*Circulation decline*). Sababu siyo teknolojia pekee, bali ni *"Content Crisis."* Msomaji hawezi kununua gazeti kusoma kile alichokiona jana kwenye TV ya serikali au kurasa za viongozi za Instagram. Gazeti linauzwa kwa "Scoops" na "Exclusives"—mambo ambayo waandishi wa sasa wanaogopa kuyaandika kwa hofu ya kutekwa au vyombo vyao kupigwa pini.

*4. Wito kwa Waziri Makonda*

Ili waandishi wasiwe masikini, Waziri asisimamie "uhuru wa maneno," bali asimamie *"Mazingira ya Uhuru wa Kiuchumi."*

* Vyombo vya habari viruhusiwe kuandika upande wa pili bila hofu ya kufungiwa. 

* Serikali iachie soko la matangazo liwe huru. 

* Sheria za habari zifanyiwe marekebisho ili mwandishi alindwe kisheria anapofichua ufisadi.

* Bodi ya Ithibati ifanye kazi yake iliyokusudiwa, kuwatambua waandishi pekee haitoshi*UCHAMBUZI: "UMASIKINI WA MWANAHABARI NI MTEGO WA MWANASIASA"*

* Bodi ya Ithibati ifanye kazi yake iliyokusudiwa, kuwatambua waandishi pekee haitoshi

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK MAGUFULI ATANGAZA KIAMA CHA MAJAMBAZI, WEZI NA MAFISADI KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI SUMBAWANGA,TUNDUMA, ILEJE NA MBOZI

VIONGOZI BORA BARANI AFRIKA KWA SASA.

UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MSALATO DODOMA KUANZA KUTUMIKA SEPTEMBA 2026

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

ASKOFU GWAJIMA: VIJANA PUUZENI WANAOCHOCHEA VURUGU