Leo nakuletea makala juu ya namna Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim alivyombana pumzi aliyekuwa Rais wa 41 wa Marekani George H.W Bush wakati huo George Bush akiwa Mwakilishi wa Kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa.
Hii ilikuwa katika Kikao cha 26 Mkutano wa 1976 uliofanyika mwaka 1971 Ajenda Kuu ikiwa ni 'Urejeshaji wa Kisheria wa Haki za Jamhuri ya Watu wa China katika Umoja wa Mataifa. Hii ilikuwa ajenda namba 93.
Kikao hiki kilikuwa ni muendelezo wa vikao vilivyokaa kwa takribani miaka 22 kujadili nafasi ya uwakilishi halali wa nchi ya China baina ya Jamhuri ya China (RoC) iliyokuwa chini ya Chiang Kai-Shek dhidi ya Jamhuri ya Watu wa China (PRC) iliyokuwa chini ya Mao Tsetung.
Kulikuwa na mgawanyiko mkubwa baina ya Marekani na Washirika wake ambao waliunga mkono uwepo wa uwakilishi wa Kai-Shek dhidi ya wale waliopinga uwakilishi huo na kutaka uwakilishi halali uwe wa Serikali ya Mao. Hawa waliongozwa na Albania.
Albania ikiongozwa na Mwakilishi wake wa Kudumu Balozi Malile na washirika wake ilipeleka Azimio Namba A/L.630 na nyongeza 1 na 2 lililotaka kutambuliwa kwa Jamhuri ya Watu wa China na Kufurushwa kwa Jamhuri ya China katika Umoja wa Mataifa.
Kwa upande wake Marekani ikiwakilishwa na George W. Bush ilipeleka Maazimio mawili A/L.632 na nyongeza 1 na 2 sambamba na Azimio Namba A/L.633 na nyongeza 1 na 2.
Marekani wao walikuwa wakitaka uwepo wa nchi mbili za China katika Umoja wa Mataifa yaani Taiwan ya Kai-Shek na China ya Mao.
Kwa upande mwingine Tunisia nao waliwasilisha Maazimio matatu A/L.639, A/L.640 na A/L. 641 ambayo yalikuwa yanafanana kwa kiasi fulani na Maazimio ya Marekani.
Kama hilo halitoshi Saudi Arabia nao waliwasilisha Azimio Namba A/L.638.
Maazimio ya Marekani, Tunisia na Saudi Arabia yalipelekwa kimkakati kwa lengo la kuvunja mpango wa Azimio la Albania na Washirika wake ikiwemo Tanzania ili usifanikiwe.
Kulikuwa na mtifuano mkubwa sana kuzuia Azimio la Albania lakini hatimaye lilikubaliwa kuwa ndiyo Azimio litakalopigiwawa kura.
Ifahamike kuwa sababu kuu ya kupeleka maazimio hayo ilikuwa ni kutaka kusifanyike upigwaji wa kura wa Azimio namba A/L. 630 na nyongeza zake 1 na 2 siku hiyo ya tarehe 25 Oktoba, 1971 na badala yake upigwaji kura ufanyike kesho yake tarehe 26 Oktoba, 1971 ili Marekani na washirika wake wajipange kuzuia Azimio hilo kupitia maazimio yao waliyoyawasilisha mezani.
Kutokana na hali ilivyokuwa Dkt. Salim Ahmed Salim alipewa majukumu mawili mahsusi, mosi kuzishawishi nchi za Afrika akiwa kama mhimili wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mataifa (African Group in the UN).
Mbali na kuzishawishi nchi za Afrika Dkt. Salim Ahmed Salim alipewa pia jukumu la kuzishawishi nchi za Asia na Latini Amerika.
Pili, Dkt. Salim Ahmed Salim alipewa jukumu la kuingilia kati jambo lolote lisilofahamika (any unknown issue) ambalo lilihitaji kuingiliwa kisheria kwa mujibu wa Kanuni za Mwenendo za Vikao vya Baraza la Umoja wa Mataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa na kuvunja kabisa mwendelezo wa jambo hilo kutoka upande wa upinzani.
Albania na washirika wake waliamini katika weledi na umahiri wa Dkt. Salim Ahmed Salim katika kuzuia aina zozote za mbinu chafu kutoka kwa Marekani na washirika wake.
Haya yalikuja kutokana na ukweli kwamba kulikuwa na habari zilianza kusambaa ndani ya viunga vya Umoja wa Mataifa kuwa Rais Nixon wa Marekani alikuwa akielekea Peking kujadiliana namna ya kuifanya Taiwan ibaki ndani ya Umoja wa Mataifa.
Hivyo mpango wa Marekani ilikuwa ni kuipa nafasi China ya Mao sambamba na ile ya Kai-Shek yaani Taiwan.
Lengo la Marekani lilikuwa kuitumia Taiwan kuikwamisha China ndani ya Umoja wa Mataifa, jambo hili Albania, Tanzania na washirika wengine walilitambua na hivyo Dkk. Salim Ahmed Salim alikuwa mtu rasmi aliyeteuliwa kufanya uingiliaji wa kimkakati (strategic intervention) kuvunja mpango huo wa Marekani.
Aidha mpango wa Marekani na Washirika wake ilikuwa ni kuchelewesha upigaji kura mpaka pale Rais Nixon atakapotoka China na hatimaye kufanikiwa mpango wao huo wa kuigawa China (kuwa China Beijing na Taiwan).
Baada ya kubaini mpango huo, Albania, Tanzania na washirika wengine walishawishi Azimio hilo lijadiliwe tarehe 25 Oktoba, 1971 badala ya tarehe ambayo inaelezwa huenda ingesubiri Rais Nixon awe amerejea kutoka Peking hivyo kuathiri mchakato huo.
Baada ya kugundua mtego huo waliotegewa nao Marekani wakashawishi Azimio la Albania lijadiliwe kuanzia saa 4 asubuhi (delaying tactics) ili walau wajipange lakini kwa bahati mbaya kwao waliwahiwa na upande wa Albania na hivyo mjadala wa China kuanza saa 3 asubuhi, hili lilikuwa pigo lingine kwa Marekani.
Mtaalamu aliyekuwa akichezesha karata hizi na kumvuruga George H.W Bush na washirika wake alikuwa si mwingine bali ni Dkt. Salim Ahmed Salim.
Baada ya kuona amekabwa koo hapumui, George H.W Bush aliomba kipengele chenye neno kuvukuzwa kwa Kai-Shek kiondolewe, George H. W Bush alisema:
"I rise to apoint of order under rule 80, to move to delete theexpulsion clause contained in the Albanian draft resolution in document A/L.630 and Add.l and 2. I refer to the concluding words of the operative paragraph of that draftresolution, which read:
" ... and to expel forthwith the representatives of ChiangKai-Shek from the place which they unlawfully occupy atthe United Nations and in all the organizations relatedto it."
Kwa tafsiri yangu isiyo rasmi, George H.W Bush alitumia mbinu ya kujifanya anakubali Azimio la Albania na kusema kuwa wataliunga mkono Azimio A/L. 630 na nyongeza zake ikiwa kipengele chenye neno kufukuzwa kwa uwakilishi wa Chiang Kai-Shek kitaondolewa katika Azimio hilo.
Mtego huu wa Marekani ilikuwa ni kuwaingiza 'kingi' Albania, Tanzania na washirika wake ili hatimaye Taiwan iweze kubaki Umoja wa Mataifa kama nchi huru huku China nayo ikiendelea kuwepo kama Mwanachama wa Kudumu wa Umoja huo.
Dkt. Salim Ahmed Salim alibaini ujanja huo wa George H.W Bush na Marekani yake na hivyo aliomba nafasi kujibu hoja, alipopewa nafasi akaendelea kumbana George H.W Bush kwa kuiainisha Kanuni ya 90 ya Kanuni za Mwenendo za Vikao vya Baraza la Umoja wa Mataifa kwa kuisoma, Dkt. Salim alisema:
"The PRESIDENT of the General Assembly has already announced the commencement of the voting. Iwant to find out from you, Mr. President, by what right the representative of the United States proposes an amendmentwhen the voting has begun? To refresh the memory of therepresentative of the United States I should like to read rule 90 of the rules of procedure:"
'After the President has announced the beginning ofvoting, no representative"-including that of the United States-"shall interrupt the voting except on a point oforder in connexion with the actual conduct of thevoting...."
Kwa tafsiri yangu isiyo rasmi ni kwamba Dkt. Salim Ahmed Salim alimbainishia George H.W Bush kuwa upigaji wa kura umelikuwa tayari hivyo haiwezekani kufanyia marekebisho Azimio ambalo tayari lipo kwenye kupigiwa kura.
Na kwa kukazia Dkt. Salim Ahmed Salim akamsomea Kanuni ya 90 ya Kanuni za Mwenendo kwamba;
'Mara tu Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa atakapotangaza upigaji wa Kura, hakuna mwakilishi, akiwemo wa Marekani (Hapa alimpiga dongo vijana wanasema) atakayeingilia upigaji kura isipokuwa kama kuna jambo la kanuni linalohusiana na upigaji kura.'
Kwa kusisitiza Rais wa Baraza hilo kwa wakati huo Adam Malik kutoka Indonesia nae akasema:
"The vote is continuing; theamendment is not receivable."
Kwamba mapendekezo ya mabadiliko yaliyotolewa na Marekani hayawezi kupokelewa.
Baada ya kuona hivyo George H.W Bush wa Marekani na washirika wake walijiona kuwa wanaelekea kushindwa katika mkakati wao huo hivyo George H.W Bush alitoa pendekezo kuwa ili Azimio lionekane kuwa limepita ni lazima lipate theluthi mbili ya kura zote.
George H.W Bush alitoa pendekezo hilo akiamini kuwa Azimio hilo la Albania lisingeweza kufika theluthi mbili lakini kwa bahati mbaya alisahau kuwa Dkt. Salim Ahmed Salim tayari alishapita kwenye kila kona kushawishi wajumbe wa Afrika, Asia na Latini Amerika.
Hatimaye Ajenda Namba 93 kuhusiana na 'Urejeshaji wa Kisheria wa Haki za Jamhuri ya Watu wa China katika Umoja wa Mataifa ikapigiwa kura kwa kuzingatia Azimio lililowekwa mezani na Albania.
Azimio hilo lilielekeza kuirejeshea China ya Mao Tse-Tung kiti chake Umoja wa Mataifa na kuifurumusha China (Taiwan) ya Kai-Shek.
Azimio hilo lilipita kwa kura 76 za ndiyo huku 35 zikilikataa na 17 zikikaa kimya na nchi tatu hazikupiga.
Huyo ndiye Dkt. Salim Ahmed Salim Mtanzania aliyemkaba koo George H.W Bush mpaka akashindwa kupumua ndani ya Baraza la Umoja wa Mataifa mwaka 1971.
Unaweza kupata rejea ya kilichojiri siku hiyo kupitia:
United Nations Digital Library ...General Assembly, 26th session 1976th plenary meeting, Monday, 25 October 1971, New York ... Action note1971-10-25. DateNew York.

Comments