*Idadi ya Sekondari ni 33:*
(i) Sekondari 31 za Kata/Serikali
(ii) Sekondari 2 za Madhehebu ya Dini (Katoliki na SDA)
*Idadi ya High Schools ni 4:*
Kasoma, Suguti, Mugango na Mtiro (mpya)
*Malengo yetu:*
(i) Sekondari kila kijiji (vijiji 68), ndani ya Kata zetu 21
(ii) High Schools 10 ifikapo Mwaka 2030, masomo ya sayansi yakipewa kipaumbele
*Sekondari mpya zitakazofunguliwa mwakani, Januari 2027:*
1. Kamatondo Sekondari
Kijiji cha Nyambono
Kata ya Nyambono
Serikali imechangia Tsh 584,280,029 (Tsh 584.28m)
Mfuko wa Jimbo umeishachangia Saruji Mifuko 250.
Wananchi na Viongozi wao, akiwemo Mbunge wa Jimbo, wanachangia ujenzi wa shule hii.
2. Rukuba Island Secondary School
Kisiwa cha Rukuba
Kata ya Etaro
Mfuko wa Jimbo umeishachangia Saruji Mifuko 300, Mabati 108 na Nondo 30
Nyansaho Foundation imechangia mabati ya rangi 130
Wananchi na Viongozi wao, akiwemo Mbunge wa Jimbo, wanachangia ujenzi wa shule hii
3. Mmahare Sekondari
Kijiji cha Mmahare
Kata ya Ifulifu
Mfuko wa Jimbo umeishachangia Saruji Mifuko 250 na Mabati ya rangi 76.
Wananchi na Viongozi wao, akiwemo Mbunge wa Jimbo, wanachangia ujenzi wa shule hii
4. Mwigombe Technical Secondary School
Kijiji cha Kiriba
Kata ya Kiriba
Wazaliwa wa Kijiji cha Kiriba, Wanakijiji na Mbunge wa Jimbo, wanachangia ujenzi wa sekondari hii ufundi.
5. Kataryo Sekondari
Kijiji cha Kataryo
Kata ya Tegeruka
Serikali imechangia Tsh milioni 100 (Tsh 100m)
Mfuko wa Jimbo umeishachangia Saruji Mifuko 100.
Wananchi na Viongozi wao, akiwemo Mbunge wa Jimbo, wanachangia ujenzi wa shule hii
*Ujenzi na uboreshaji wa sekondari Jimboni mwetu:*
(i) Tuendelee kuchangia ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi kwenye sekondari zetu za zamani.
(ii) Tuendelee kuchangia ujenzi wa sekondari mpya za Kidato I-IV, zikiwemo za ufundi
(iii) Tuendelee kujenga "high schools" mpya za masomo ya sayansi.
*Picha iliyoambatanishwa hapa:* Wananchi wa Kijiji cha Mmahare, Kata ya Etaro wakijenga sekondari ya kijiji chao. Ifikapo Januari 2027, Kata hii yenye vijiji vinne (4) itakuwa na sekondari tatu (3) vijijini Etaro, Mmahare na Kisiwani Rukuba.
*Shukrani:* Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini na Viongozi wao wa ngazi zote wanaendelea kutoa shukrani nyingi mno kwa Serikali yetu inayoongozwa vizuri na *Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan* kwa kuendelea kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo ya Jimboni mwetu - ahsante sana!
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Date: Thu, 2 July 2026

Comments