MAKONDA AJIONEA MAKUBWA ALIPOTEMBELEA PARIS FC UFARANSA

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda leo July 08,2026 ametembelea klabu kubwa nchini Ufaransa ya Paris FC kwa lengo la kukuza ushirikiano wa Tanzania na klabu hiyo na kuongeza wigo mpana wa fursa ya kukuza soka la Tanzania hususani kupitia Timu za Taifa na pia kuwawezesha Vijana wa Tanzania kucheza klabu za ulaya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maono ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan 


Makonda akiwa Paris FC amepokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo, Fabrice Herrault ambapo pamoja na kujadiliana fursa za kubadilishana uzoefu katika kukuza maendeleo ya soka kuelekea AFCON 2027, uongozi wa Paris FC umemkabidhi Waziri Makonda jezi yake na jezi yenye jina la Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kama sehemu ya kutambua mchango wake mkubwa wa kukuza soka na michezo kwa ujumla nchini Tanzania.

Makonda amesema “Tumetembelea klabu kubwa Ufaransa na Bara la Ulaya, Paris FC ni Wazawa wa Jiji la Paris, ni timu kubwa yenye mafanikio makubwa kuanzia timu ya Wanawake hadi timu za Vijana na ndio Washindani wakubwa wa PSG yaani ukisiki mechi ya PSG vs Paris FC una uhakika Paris FC inawatoa jasho PSG, ni timu kubwa ina miaka mingi”

“Tumetembelea leo na menejimenti imetukaribisha na lengo letu kubwa ni kuangalia fursa ya ushirikiano kati ya timu zetu za Tanzania hususani timu za Taifa na club ya Paris FC na tuna matumaini makubwa kwasababu kazi nzuri wanayoifanya tunatumaini Tanzania siku moja tutavuka mipaka ya Afrika na kuja Ulaya”

“Ni ndoto ya Rais Samia kuwaona Watoto wake wa Tanzania wakicheza timu za Ulaya, na Ufaransa ni mlango wa kuingia timu za Ulaya na sisi tumeutafuta huu mlango, mazungumzo yanaendelea na wametupa zawadi ikiwemo jezi ya kumpelekea zawadi Rais Samia wakifahamu ni Mwanamke ambaye ni Champion wa Sports na Mimi namuhakikisha Mh. Rais na Watanzania wakati umefika wa Taifa letu kuinuka kwenye michezo, nimewaomba Diaspora waendelee kutuonesha fursa zilizopo katika Dunia ili tuzitumie kujenga mustakabali mpana wa Taifa letu, tunahitaji Watanzania wacheze Paris FC”



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK MAGUFULI ATANGAZA KIAMA CHA MAJAMBAZI, WEZI NA MAFISADI KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI SUMBAWANGA,TUNDUMA, ILEJE NA MBOZI

PICHA YA RAIS ILIYOBAMBA WIKI HII

JUA AINA NNE ZA KABILA LA WASUKUMA

18 WAPITISHWA KUGOMBEA UONGOZI YANGA

VIONGOZI BORA BARANI AFRIKA KWA SASA.

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

ZIJUE SIFA ZA WANYAKYUSA WA KYELA NA RUNGWE