Misri imezindua Makao Makuu Makubwa zaidi ya Kijeshi Duniani, yakiipita Pentagon ya Marekani.
Himaya mpya ya Wizara ya Ulinzi ya Misri, inayojulikana kama Octagon si kikubwa zaidi barani Afrika tu, bali pia imeipita Pentagon ya Marekani na kuwa kituo kikubwa zaidi cha makao makuu ya ulinzi duniani.
Makao hayo Makuu ya amri ya Serikali yanatumika pia kama Wizara ya Ulinzi ya Misri mradi unaowakilisha hatua kubwa ya uhuru kwa vikosi vya jeshi vya nchi hiyo.
Mji huo mkuu mpya wa jeshi la Misri upo jangwani yapata kilomita 45 mashariki mwa Cairo ukiwa na ukubwa wa takriban hekari 22,000, na eneo la sakafu la zaidi ya futi za mraba milioni 50.5.
Eneo hilo lina majengo manane ya umbo la pembe nne (yanayojumuisha Jeshi, Jeshi la Wanamaji, Jeshi la anga na Ulinzi wa anga) na ni kituo cha amri kilichojengwa ili kuhifadhi taasisi muhimu za eneo hilo zima.

Comments