Ndege ya kwanza ya Shirika la Ndege Tanzania (Air Tanzania) ya safari za moja kwa moja kutoka Tanzania imewasili jana mjini Moscow, Urusi, ikitekeleza mpango uliotangazwa na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Safari hiyo inaunganisha Dar es Salaam, Zanzibar na Moscow, hatua inayotarajiwa kuimarisha usafiri wa anga kati ya Tanzania na Urusi.
Hatua hiyo pia inalenga kukuza biashara, utalii na uwekezaji kati ya mataifa hayo mawili. Wakati huohuo, Serikali inaendelea na mipango ya kuendeleza bandari ya usafirishaji mizigo katika eneo la Mangapwani, Zanzibar, ili kuongeza ufanisi wa biashara na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa.

Comments