NGORONGORO HAKUNA KULALA SABASABA.


NA MWANDISHI WETU

TUKIO la Ngorongoro kuonesha vivutio vya utalii mubashara kupitia runings kubwa iliyofungwa katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii

limevutia wananchi wengi wanaotembelea  maonesho ya 50 ya biashara ya kimataifa jijini  Dar es Salaam kwa kuoneshwa maajabu yaliyopo Ngorongoro hususan Kreta ya Ngorongoro, makundi ya wanyama mbalimbali ikijumuisha pundamilia, nyumbu, swala, nyati na wanyama adimu kama  faru, simba, tembo na  na  chui na kujihisi kama wapo nyumbani Ngorongoro.


Ofisa Uhusiano Mkuu wa Ngorongoro  Walter Mairo ameeleza kuwa  kupitia runinga iliyofungwa viwanja vya maonesho wageni wanaotembelea wanaona wanyama aina mbalimbali ndani ya Kreta, tambarare za Ndutu ambapo maisha ya Nyumbu kuzaliwa, kukua, kusafiri na kurejea na kuanza kizazi kipya kila mwaka


Mairo ameongeza kuwa, matukio mubashara yanaonesha wananchi jinsi teknolojia ya kidigitali na utalii wa asili vinavyoweza kushirikiana kuelimisha, kuburudisha na kuonyesha ushahidi kuwa Ngorongoro si tu hifadhi, bali ni jukwaa la kidunia linalounganisha urithi, biashara na teknolojia sehemu moja.


Karibu Sabasaba timu yetu yenye wabobezi na watopezi imejipanga kukupa  hadhithi za Ngorongoro zitakazokuduwaza kuwa Ngorongoro sio mahali pa kuangalia tu, bali mahali pa kuelewa, kujifunza na kuishi uzoefu usiosahaulika.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK MAGUFULI ATANGAZA KIAMA CHA MAJAMBAZI, WEZI NA MAFISADI KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI SUMBAWANGA,TUNDUMA, ILEJE NA MBOZI

PICHA YA RAIS ILIYOBAMBA WIKI HII

JUA AINA NNE ZA KABILA LA WASUKUMA

18 WAPITISHWA KUGOMBEA UONGOZI YANGA

VIONGOZI BORA BARANI AFRIKA KWA SASA.

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

ZIJUE SIFA ZA WANYAKYUSA WA KYELA NA RUNGWE