NMB NMB YASOGEZA BIMA KIDIGITALI KUPITIA UMEBIMA MINI APP

Benki ya NMB imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za bima kidijitali kupitia Umebima Mini App, huduma iliyounganishwa ndani ya programu ya NMB Mkononi, inayowawezesha wateja kununua bima kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi.

Akizungumza na waandishi wa habari, katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, maarufu kama Sabasaba, Mkuu wa Idara ya Bima Benki ya NMB, Martin Massawe, alisema huduma hiyo inaendana na kauli mbiu ndogo ya maonesho hayo, “Biashara za Tanzania Kidijitali Zaidi.”

Massawe alisema Umebima Mini App imeondoa ulazima wa mteja kufika tawi la benki au ofisi za bima, kwa kuwa sasa anaweza kuchagua na kununua bima inayokidhi mahitaji yake akiwa mahali popote, kwa njia rahisi, salama na ya haraka kupitia NMB Mkononi.

Alisema bima ni nyenzo muhimu ya usalama wa kifedha kwa mtu binafsi, familia na biashara, hasa katika kujikinga dhidi ya majanga yasiyotegemewa. Aliongeza kuwa NMB imeandaa bidhaa mbalimbali za bima kwa makundi tofauti, ikiwemo Matching Insurance kwa wafanyabiashara wadogo, ili kusaidia kulinda biashara zao kwa gharama nafuu na kupitia njia za kidijitali.





 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK MAGUFULI ATANGAZA KIAMA CHA MAJAMBAZI, WEZI NA MAFISADI KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI SUMBAWANGA,TUNDUMA, ILEJE NA MBOZI

VIONGOZI BORA BARANI AFRIKA KWA SASA.

ZIJUE SIFA ZA WANYAKYUSA WA KYELA NA RUNGWE

18 WAPITISHWA KUGOMBEA UONGOZI YANGA

PICHA YA RAIS ILIYOBAMBA WIKI HII

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

NMB, CTM TANZANIA WAZINDUA MIKOPO YA KUMALIZIA NYUMBA