NMB YARAHISISHA USIMAMIZI WA VIKUNDI KUPITIA KIKUNDI MINI APP

 Benki ya NMB imesema huduma ya NMB Kikundi Mini App, iliyopo ndani ya NMB Mkononi Super App, imebuniwa kurahisisha usimamizi wa vikundi kwa kuwawezesha wanachama na viongozi kupata huduma za kifedha kidigitali kwa usalama, uwazi na ufanisi zaidi.


Akizungumza katika Banda la NMB kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, maarufu Sabasaba, Meneja wa Kanda, Huduma za Vikundi na Benki Vijijini wa NMB, Dismas Prosper, alisema mfumo huo unapunguza muda na gharama za kupata huduma za benki, huku ukiimarisha usalama wa miamala na kurahisisha shughuli za vikundi mbalimbali vya kijamii na kiuchumi.

Prosper alisema kupitia NMB Kikundi Mini App, wanachama wa vikundi wanaweza kufungua akaunti bila kutembelea tawi la benki, kufanya miamala kwenda benki nyingine na mitandao ya simu, pamoja na kuweka michango yao moja kwa moja kwenye akaunti ya kikundi. Aidha, alisema kila mwanachama hupokea ujumbe mfupi wa simu unaothibitisha mchango uliowekwa, hatua inayoongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa fedha za kikundi.

Aliongeza kuwa mfumo huo pia unawawezesha wanachama kuona taarifa za hisa, idadi na majina ya wanachama wa kikundi, pamoja na taarifa binafsi za kila mwanachama kulingana na mamlaka aliyopewa ndani ya mfumo. Prosper alisema ubunifu huo ni sehemu ya jitihada za NMB kuendelea kuleta suluhisho za kidigitali zinazowawezesha wananchi, hususan vikundi vya kijamii na kiuchumi, kupata huduma za kifedha kwa urahisi, usalama na uwazi zaidi.









Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK MAGUFULI ATANGAZA KIAMA CHA MAJAMBAZI, WEZI NA MAFISADI KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI SUMBAWANGA,TUNDUMA, ILEJE NA MBOZI

JUA AINA NNE ZA KABILA LA WASUKUMA

PICHA YA RAIS ILIYOBAMBA WIKI HII

18 WAPITISHWA KUGOMBEA UONGOZI YANGA

VIONGOZI BORA BARANI AFRIKA KWA SASA.

ZIJUE SIFA ZA WANYAKYUSA WA KYELA NA RUNGWE

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA