Takribani wiki moja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanya ziara nchini Urusi, mamia ya watalii wameanza kuwasili nchini kutembelea vivutio vya utalii.
Akizungumza na vyombo vya Habari ndani ya ndege Boeing 787-8 Dreamliner ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) iliyokuwa ikitokea Urusi kuelekea Tanzania Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji, amesema Ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi katika sekta ya utalii umeanza kuzaa matunda kufuatia kutiwa saini kwa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya nchi hizo mbili, hatua inayofungua ukurasa mpya wa ushirikiano katika kukuza utalii na kuimarisha diplomasia ya uchumi.
Dkt. Kijaji amesema mafanikio hayo ni matunda ya jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kufungua masoko mapya ya utalii ili kuleta matokeo chanya, huku safari ya kwanza ya ndege hiyo ikishuhudia mwitikio mkubwa kutoka kwa wasafiri na watalii wa Urusi.
Ameongeza kuwa Hati ya Makubaliano iliyosainiwa kati ya Tanzania na Urusi inatarajiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya watalii kutoka Urusi, ambapo lengo ni kufikia kati ya watalii 200,000 hadi 500,000 ifikapo mwisho wa mwaka 2026, kutoka takribani watalii 17,000 waliokuwa wakitembelea Tanzania hapo awali.
Dkt. Kijaji pia amesema mawakala wa utalii walioambatana na ujumbe wa Serikali katika ziara ya kibiashara (Business to Business – B2B) wamepongeza hatua ya Serikali ya kuwaunganisha na wafanyabiashara wa Urusi, wakieleza kuwa hatua hiyo imefungua fursa mpya za biashara na kuongeza ushindani wa Tanzania katika soko la utalii la kimataifa.
Kwa upande wake, mmoja wa watalii aliyewasili nchini kutoka Urusi, Ola Vlandamir, amesema alivutiwa kusafiri kwenda Tanzania baada ya kuona matangazo kuhusu safari hiyo kupitia vyombo vya habari.
Amesema katika ziara yake anatarajia kutembelea Zanzibar pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ili kujionea vivutio vya kipekee vya utalii ambavyo Tanzania imebarikiwa kuwa navyo.
Mafanikio hayo yanaendelea kuthibitisha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuimarisha sekta ya utalii kwa kufungua masoko mapya ya kimataifa kuongeza idadi ya watalii.
𝗠𝗮𝗸𝗮𝗯𝗶𝗹𝗮 10 𝗮𝗺𝗯𝗮𝘆𝗼 𝘂𝗸𝗶𝗸𝗮𝗮 𝗸𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝗻𝗮𝗼, 𝗸𝘂𝘁𝗼𝗯𝗼𝗮 𝗸𝘂𝗻𝗮𝘄𝗲𝘇𝗮 𝗸𝘂𝘄𝗮 𝗿𝗮𝗵𝗶𝘀𝗶 𝘇𝗮𝗶𝗱𝗶 ⚠️ Kumbuka: Haya ni maoni na mitazamo ya kijamii tu, si kwamba kabila fulani lina mafanikio kuliko lingine. Mafanikio yanategemea juhudi, elimu, nidhamu na fursa. 1. Wasukuma Wana sifa ya kufanya kazi kwa bidii, hasa kwenye kilimo, ufugaji na biashara. Wengi huaminika kuwa wavumilivu katika kutafuta maendeleo. 2. Wachagga Hujulikana kwa moyo wa biashara, uwekezaji na kusaidiana kifamilia katika shughuli za maendeleo. 3. Wahaya Wana historia ndefu ya biashara, elimu na shughuli za uzalishaji zinazochochea maendeleo. 4. Wanyakyusa Wengi wanasifiwa kwa bidii katika biashara, kilimo na uwekezaji wa muda mrefu. 5. Wakinga Hujulikana kwa uchapakazi, nidhamu na uthubutu wa kutafuta fursa sehemu mbalimbali za nchi. 6. Waha Wana sifa ya kujituma katika biashara na shughuli mbalimbali za kiuchumi. 7. Wapare Mara nyingi husifiwa kwa kuthamini elimu, kazi na mipango y...
Comments