‎WAJASIRIAMALI ZAIDI YA 1,000 WAHITIMU MAFUNZO YA 'JIFUNZE KWA MAMA UJASIRIAMALI' MOROGORO

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

‎Afisa Maendeleo wa Mkoa wa Morogoro, Gibson Mwakoba, amesema ameridhishwa na mwitikio mkubwa wa wajasiriamali zaidi ya 1,000 waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali ya "Jifunze kwa Mama Ujasiriamali" kwa siku tatu mfululizo bila kukata tamaa.

‎Mafunzo hayo yaliandaliwa na Jukwaa Huru la Wahariri Tanzania (JUWATA) kwa kushirikiana na Taasisi ya MAMO Entrepreneurship, na yalifanyika katika Ukumbi wa Bwalo la JKT Umwema, Morogoro Mjini, kuanzia Julai 13 hadi 15, 2026.

‎Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo akiwa mgeni rasmi, Mwakoba aliwapongeza viongozi wa JUWATA na MAMO Entrepreneurship kwa maandalizi mazuri yaliyowezesha mafunzo hayo kufanyika kwa mafanikio makubwa na kuwajengea washiriki ujuzi wa kujiajiri na kukuza biashara zao.

‎Kwa upande wake, Mwenyekiti wa JUWATA, Richard Mwaikenda, alitoa shukrani kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, kwa kuunga mkono mafunzo hayo kwa kutuma wawakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Alisema wakati wa ufunguzi, Mkoa uliwakilishwa na Katibu Tawala  sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Beatrice Njawa, huku hafla ya kufunga ikiongozwa na Afisa Maendeleo wa Mkoa, Gibson Mwakoba.

‎Naye Mkurugenzi wa MAMO Entrepreneurship, Mohamed, alisema washiriki walipata mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali yaliyolenga kuwawezesha kujitegemea kiuchumi.

Pia aliziomba mamlaka za Mkoa wa Morogoro kuwapa kipaumbele wahitimu hao katika upatikanaji wa mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri, akieleza kuwa tayari wamehitimu mafunzo na kukabidhiwa vyeti.

‎Mbali na mafunzo hayo, JUWATA ilitumia fursa hiyo kulitambulisha rasmi Jukwaa hilo kwa wadau mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ya habari na jamii katika kuhamasisha maendeleo kupitia elimu na ujasiriamali.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Soma Taarifa ya UTEUZI:Rais Jakaya Kikwete amemteua Dkt. Ben E. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya PUMA Energy (zamani ilijulikana kama BP Ltd)

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK MAGUFULI ATANGAZA KIAMA CHA MAJAMBAZI, WEZI NA MAFISADI KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI SUMBAWANGA,TUNDUMA, ILEJE NA MBOZI

MAAFISA JENERALI WASTAAFU 17 WA JWTZ WAAGWA.

PICHA YA RAIS ILIYOBAMBA WIKI HII

18 WAPITISHWA KUGOMBEA UONGOZI YANGA

JUA AINA NNE ZA KABILA LA WASUKUMA

BINTI WA KITANZANIA GLORIA MAJULE ASHINDA TUZO YA UANDISHI BORA WA FILAMU YA MALARIA MAREKANI ‎