WANAKIJIJI WAENDELEA NA UJENZI WA SEKONDARI YAO YA UFUNDI

Mwigombe Technical Secondary School, Kijijini Kiriba, Musoma Vijijini

Wanakijiji wakishirikiana na Wazaliwa wa Kijiji cha Kiriba, Jimbo la Musoma Vijijini, wanaendelea na ujenzi wa sekondari ya ufundi ambayo itawekewa Jiwe la Msingi na Mwenge wa Uhuru tarehe 8.8.2026

Michango ya ujenzi wa sekondari hiyo:
(i) Wanakijiji
(ii) Familia Mashenene 
(iii) Baadhi ya wazaliwa wa Kata ya Kiriba
(iii) Mbunge Prof Muhongo 
(iv) Wadau wa Maendeleo: benki za CRDB & NMB

Miundombinu itakayokuwa imekamilika ifikapo tarehe 4.8.2026

(i) Jengo lenye vyumba 2 vya madarasa na ofisi 1 katikati
(ii) Jengo lenye nyumba 2 vya madarasa
(iii) Choo chenye matundu 5

Ujenzi unaendelea kwa kasi kubwa ili sekondari hiyo ifunguliwe Januari 2027.

Alhamisi, 6.8.2026: Sherehe Kijijini Kiriba, Kata ya Kiriba

Wanakijiji wa Kijiji cha Kiriba watafanyiwa sherehe na Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo ikiwa ni kuwapongeza kwa juhudi zao za kujitolea kuchangia maendeleo yao wakishirikiana na Serikali yetu

Mafanikio yatakayosherehekewa:

(i) Ujenzi wa Sekondari ya Ufundi ya Mwigombe kijijini hapo

(ii) Ujenzi wa Zahanati mpya kijijini hapo. Serikali imechangia Tsh 259,000,000 (Tsh 259m), na Wanakijiji wamechangia nguvukazi

Shukrani:
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini na Viongozi wao wa ngazi zote wanaendelea kuishukuru sana Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kugharamia miradi ya maendeleo ya Jimboni mwetu - ahsante sana.

Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha ujenzi unaoendelea kwenye Mwigombe Technical Secondary School ya kijijini Kiriba, Kata ya Kiriba, Musoma Vijijini 

Ofisi ya Mbunge 
Jimbo la Musoma Vijijini 
www.musomavijijini.or.tz 

P. O. Box 6
Musoma

Date: Fri, 31.7.2026







 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KATIKA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA.

YANGA YAMPOTEZA MAMA FATMA KARUME MWANA YANGA KINDAKI NDAKI

SERIKALI ITAENDEA KUHIMIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI- LONDO

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA