WAZIRI NDEJEMBI AJADILI AWAMU YA PILI YA MRADI WA UMEME WA JUA KISHAPU NA WASHIRIKA WA MAENDELEO


NA MWANDISHI WETU, PARIS UFARANSA

WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi kutoka Wizara ya Fedha ya Ufaransa, Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) pamoja na kampuni ya SAGECOM, kwa lengo la kujadili utekelezaji wa awamu ya pili ya Mradi wa Uzalishaji Umeme wa Jua wa Megawati 100 unaotekelezwa katika Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga.


Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Julai 6, 2026, katika Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Paris, Ufaransa.


Katika kikao hicho, Ndejembi ameishukuru Serikali ya Ufaransa kupitia Wizara yake ya Fedha na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) kwa kuendelea kuwa mshirika muhimu wa Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya sekta ya nishati. Amesema ushirikiano huo umeendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha upatikanaji wa nishati ya uhakika na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa AFD,  Sandra Kassab, ameipongeza Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati kwa hatua kubwa iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi ya nishati, hususan ile inayolenga kuongeza uzalishaji wa umeme na kuimarisha matumizi ya nishati safi.


 Aidha, ameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa ufanisi na kuleta manufaa kwa wananchi wa Tanzania.





Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK MAGUFULI ATANGAZA KIAMA CHA MAJAMBAZI, WEZI NA MAFISADI KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI SUMBAWANGA,TUNDUMA, ILEJE NA MBOZI

JUA AINA NNE ZA KABILA LA WASUKUMA

PICHA YA RAIS ILIYOBAMBA WIKI HII

18 WAPITISHWA KUGOMBEA UONGOZI YANGA

VIONGOZI BORA BARANI AFRIKA KWA SASA.

ZIJUE SIFA ZA WANYAKYUSA WA KYELA NA RUNGWE

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA