Winga wa kimataifa wa Tanzania ๐น๐ฟ, Hasnath Ubamba amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Madrid Club de Fรบtbol Femenino (Madrid CFF) inayoshiriki ligi kuu ya wanawake nchini Uhispania .
Kabla ya uhamisho huu wa kihistoria kwenda Uhispania, Ubamba alikuwa akicheza soka la kulipwa katika klabu ya FC Masar nchini Misri. Akiwa nchini Misri, alionyesha kiwango cha juu sana ikiwemo kusaidia timu yake kumaliza nafasi ya tatu kwenye michuano ya klabu bingwa ya wanawake ya CAF na kuibuka miongoni mwa washambuliaji bora .
Ubamba anaejulikana kwa kasi, utulivu anapokuwa na mpira mguuni, umahiri wa kufunga na kutoa pasi za mwisho (assists). Kabla ya kujiunga na soka la kulipwa nje ya nchi, aliwahi kung'aa katika klabu ya Fountain Gate Princess ya Tanzania .
Katika msimu uliomalizika wa 2025|26, Hasnath Ubamba, alifunga mabao 15 na kutoa pasi za mwisho (assists) 7 katika michuano yote aliyoshiriki akiwa na kikosi cha FC Masar licha ya kukosa baadhi ya michezo kutokana na majeraha .
๐ | TAKWINU ZA MUDA WOTE
Hasnath Ubamba katika kipindi chote akiwa na klabu ya FC Masar (2024 - 2026) .
◉ 62 Games (all competitions)
◉ 30 Goals
◉ 19 Assists
◉ 49 G/A

Comments