Makundi maalumu 27,946 yamesajiliwa kwenye mfumo wa NeST na kupata zabuni zenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 56, kupitia Mfumo huo.makundi ya vijana ni 13, 317 wanawake 13,400, wazee 643 na watu wenye ulemavu 586.

Hayo yemebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dennis Simba wakati wa mkutano na vyombo vya habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO, katika Mji wa Serikali wa Mtumba jijini Dodoma, Agosti 20, 2026.   

  

Sheria ya Ununuzi wa Umma, imezielekeza taasisi zote za umma kutenga asilimia 30 ya bajeti zao za ununuzi kwa ajili ya makundi maalum (vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu).

 


Lengo la PPRA, kwa kuzingatia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ni kuwa na takribani makundi 300,000 yaliyo tayari kuomba zabuni. Hatua hii ni sehemu ya jitihada za Serikali kutoa ajira na kazi kwa Watanzania ambao hawana uwezo wa kuwa na kampuni, ambao wanaweza kujiunga kwenye vikundi na kutekeleza zabuni husika. ร  Riple effect ya kazi na ajira 3,000,000

 

Kutokana na nia ya kuwainua Watanzania kiuchumi, Kundi maalum linaweza kupata zabuni moja yenye thamani ya hadi Shilingi Milioni 500.

 

Kutokana na umuhimu wa suala hili, Serikali imeliweka kuwa sehemu ya ajenda muhimu kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu. Hatua iliyoongeza usajili wa vikundi, hamasa na utekelezaji wa utoaji wa zabuni. Na hapa nichukue fursa hii kuishukuru Ofisi ya Rais – Wizara ya Maendelea ya Vijana kwa kuridhia ombi letu la kushhirikiana nao kwenye jambo hili ambapo tutazunguka nao katika Halmashauri zote 184 nchini.

 

Hivyo, tunawasihi Watanzania tuendelee kujiunga kwenye vikundi vya watu watatu na kuendelea, kuvisajili kwenye Halmashauri zao, na kisha wasajili kwenye Mfumo wa NeST ambao ndio wenye zabuni zote za umma. Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa tunakuwa na uchumi jumuishi; kwamba kila Mtanzania ananufaika na anachangia pia kwenye ukuaji wa uchumi katika ngazi yoyote aliyopo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUAPISHWA NDEJEMBI KUWA MAKAMU WA RAIS

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

NI MAKOSA WANAFUNZI KUFIKA SHULE SAA 1:15 ASUBUHI

URUSI, CHINA, IRANI NA KOREA KASKAZINI WAPANGA KUUNDA JESHI MOJA LA KUJIHAMI

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€

PANYA MAGAWA WA SUA TANZANIA AJENGEWA MNARA WA HESHIMA CAMBODIA