NI MAKOSA WANAFUNZI KUFIKA SHULE SAA 1:15 ASUBUHI

Wizara ya Elimu imewakumbusha waendesha shule nchini kuzingatia sheria inayowataka wanafunzi kufika shule saa 2:00 asubuhi (8:00 AM), huku ikisisitiza kuwa hakuna shule inayoruhusiwa kuwalazimisha wanafunzi kufika mapema zaidi ya muda huo.

Kwa mujibu wa Kanuni 84 ya Sheria ya Elimu ya Msingi ya 2015, saa 2:00 asubuhi ndio muda uliopangwa wa wanafunzi kuanza shughuli zao za shule, huku muda wa saa 1:15 asubuhi (7:15 AM) ukiwa ni muda wa mapema zaidi unaoruhusiwa kwa ajili ya maandalizi kabla ya masomo kuanza na sio chini ya hapo.

Wizara imeonya kuwa itachukua hatua kali dhidi ya shule zitakazobainika kukiuka sheria hiyo kwa kuwalazimisha wanafunzi kufika mapema sana, huku ikisisitiza kuwa muda huo umewekwa ili kulinda afya na ustawi wa wanafunzi na kuhakikisha wanapata usingizi wa kutosha usiku.


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KATIKA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA.

YANGA YAMPOTEZA MAMA FATMA KARUME MWANA YANGA KINDAKI NDAKI

𝐌𝐉𝐔𝐄 𝐊𝐀𝐂𝐇𝐄𝐑𝐎 𝐌𝐙𝐄𝐍𝐀

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA