Mama Fatma Karume, aliyekuwa mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, amefariki dunia leo hii.Taarifa za kifo chake zimefika wakati akiwa nyumbani kwa Mmoja ya watoto wake huko Zanzibar.
Mama Fatma Karume alikuwa mjane wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar, ambaye aliongoza Zanzibar baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964.
Kifo chake kinatajwa kuwa ni msiba mkubwa kwa familia, ndugu, jamaa na wananchi wa Zanzibar, huku taarifa zaidi kuhusu mazishi na ratiba nyingine za msiba zikitarajiwa kutolewa na Serikali. Mama Fatma Karume anafariki akiwa na umri wa miaka 97.

Comments