MRI KIGANJANI, UBUNIFU WA AI KWA AFYA



Je, inawezekana kupata picha zinazofanana na MRI bila mgonjwa kuingia kwenye mashine ya MRI?


Ndiyo! MRI Kiganjani ni ubunifu unaotumia Akili Unde (AI) unaolenga kusaidia kukabiliana na changamoto za magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa binadamu na wanyama.


Akiwasilisha ubunifu huo katika Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu mkoani Tanga, Dkt. Jamal Firmat Banzi, Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), amesema teknolojia hiyo ina uwezo wa kuzalisha picha zenye ufanano wa hadi asilimia 92 na picha zinazopatikana kupitia MRI halisi.


Teknolojia hii inaweza kusaidia:

• Kupata majibu ya vipimo kwa haraka zaidi

• Kuongeza utayari wa watu kufanya vipimo vya MRI

• Kupunguza gharama za huduma za afya

• Kusaidia kutambua viashiria vya magonjwa kama Kiharusi (Stroke) na Dementia mapema


Kwa mujibu wa maelezo ya ubunifu huo, AI inaweza kusaidia kutambua viashiria vya magonjwa hayo miaka 10–15 kabla ya dalili kuonekana, jambo linaloweza kutoa fursa kwa wataalamu wa afya kuchukua hatua mapema.


Ubunifu wa Kitanzania, teknolojia kwa afya bora. 


#MRIKiganjani #AI #Ubunifu #Afya #Teknolojia #Innovation #Tanzania #SUA #NCDs



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KATIKA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA.

YANGA YAMPOTEZA MAMA FATMA KARUME MWANA YANGA KINDAKI NDAKI

𝐌𝐉𝐔𝐄 𝐊𝐀𝐂𝐇𝐄𝐑𝐎 𝐌𝐙𝐄𝐍𝐀

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA