WAZIRI Mkuu mstaafu Mizengo Pinda amewapongeza wadau na wakulima wanaofuata mbinu za kilimo ikolojia kwa kuwa kina tija kwenye jamii na uchumi.
Pinda ambaye tangu astaafu amejikita kwenye kilimo, ameonesha kufurahishwa na mwamko wa wakulima kujikita na kilimo ikolojia.
Washiriki wa banda la kilimo ikilojia wameonesha mbegu, viuatilifu na mbolea mbalimbali ambazo ni asili na salama.
Banda hilo limeshirikisha Mtandao wa Baionuwai Tanzania (TABIO), Shirila la Island of Peace (IDP), Mwavuli wa Kilimo Hai Tanzania (TOAM), Shirikisho la Vyama vya Wakulima na Wafugaji Tanzania (SHIWAKUTA), Kitovu cha Kilimo Ikolojia Tanzania (Agroecology HUB) na SWISS AID.
![]() |
.jpg)




Comments