TAMISEMI, UDSM KUIMARISHA USHIRIKIANO WA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MIUNDOMBINU

 


NA MWANDISHI WETU, DODOMA

NAINU Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila, amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kuhusu kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi inayosimamiwa na Ofisi hiyo.


Katika kikao hicho, pande hizo zimejadili maeneo ya ushirikiano, hususan matumizi ya utaalamu, teknolojia na uzoefu wa kitaasisi katika kuhakikisha miradi ya miundombinu inatekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa, kwa wakati na kuleta thamani halisi kwa wananchi.


Mhandisi Mativila amesisitiza umuhimu wa taasisi za Serikali kushirikiana na vyuo vikuu katika kupata suluhisho za kitaalamu zitakazosaidia kuongeza ufanisi na ubora wa miradi ya ujenzi inayotekelezwa nchini.


Kwa upande wake, Mkuu wa Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Innocent Macho, alisema Chuo hicho kina uwezo na uzoefu mkubwa wa kutoa huduma za kitaalamu kupitia kampuni yake ya ushauri, The Bureau for Industrial Cooperation (BICO), ambayo imeshiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.


Pande hizo zimekubaliana kuendelea na majadiliano ili kuweka mazingira madhubuti ya ushirikiano yatakayochangia utekelezaji bora na endelevu wa miradi ya miundombinu chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI.





Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

Soma Taarifa ya UTEUZI:Rais Jakaya Kikwete amemteua Dkt. Ben E. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya PUMA Energy (zamani ilijulikana kama BP Ltd)

VIONGOZI NA WATENDAJI WA MATAWI UVCCM PANGANI WANOLEWA

NMB YAWAUNGANISHA WANANCHI NA HUDUMA, FURSA ZANZIBAR

HIZI HAPA TAKWIMU ZA PETER SHALULILE MCHEZAJI MPYA WA YANGA SC 🔰 🔥