TANZANIA YANG’ARA KWA MARA YA KWANZA MBIO ZA VIHUNZI FEASSA 2026


NA OWM TAMISEMI, MOROGORO


Tanzania imeandika historia katika Mashindano ya FEASSA Games 2026 baada ya kushiriki kwa mara ya kwanza katika mbio za kuruka vihunzi na kufanikiwa kutwaa nafasi ya tatu.


Mashindano hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, yameshuhudia wanariadha wa Tanzania wakionesha ushindani mkubwa na kupeperusha vyema bendera ya Taifa.


Katika mbio hizo, Magrita IQamunga alimaliza katika nafasi ya tatu, huku Winfrida Urbano akishika nafasi ya nne, matokeo yanayoonesha uwezo na vipaji vinavyoendelea kukua katika riadha nchini.


Mafanikio hayo yameongeza hamasa kwa Tanzania katika FEASSA Games 2026, huku ushiriki wa kwanza katika mbio za vihunzi ukiwa hatua muhimu katika kukuza na kuibua vipaji vipya vya riadha miongoni mwa wanafunzi.


Tanzania inaendelea kuonesha ushindani katika michezo mbalimbali ya FEASSA 2026, huku vijana wakipeperusha bendera ya Taifa kwa bidii, nidhamu na ari ya ushindi.




Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Soma Taarifa ya UTEUZI:Rais Jakaya Kikwete amemteua Dkt. Ben E. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya PUMA Energy (zamani ilijulikana kama BP Ltd)

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

VIONGOZI NA WATENDAJI WA MATAWI UVCCM PANGANI WANOLEWA

NMB YAWAUNGANISHA WANANCHI NA HUDUMA, FURSA ZANZIBAR

HIZI HAPA TAKWIMU ZA PETER SHALULILE MCHEZAJI MPYA WA YANGA SC 🔰 🔥

KAMATI YA BUNGE PAC YABAINI MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA UMMA MZUMBE