TARURA WAPATIWA MAFUNZO YA MATUMIZI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA


NA MWANDISHI WETU DODOMA

WAKALAya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imepatiwa mafunzo kuhusu matumizi ya taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara za wilaya nchini.


Akizungumza wakati wa mafunzo hayo kwa watendaji wa TARURA, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang’a amesema ni muhimu usanifu na utekelezaji wa miundombinu ya barabara kuzingatia taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka hiyo.


Amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo watendaji wa TARURA kutumia taarifa za hali ya hewa hususan utabiri wa msimu wa mvua ili kuwezesha kuchukua tahadhari mapema na kupanga kwa ufanisi shughuli za ujenzi na matengenezo ya barabara.


Dkt. Chang’a amesema matumizi sahihi ya taarifa hizo yatasaidia kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na hali mbaya ya hewa na kuongeza ufanisi na uimara wa miundombinu ya barabara nchini.


Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff ameishukuru TMA kwa kutoa mafunzo hayo, amesema elimu hiyo itawawezesha watendaji wa Wakala kutumia taarifa za hali ya hewa katika usanifu, ujenzi na matengenezo ya barabara za wilaya nchini.


Amesema ushirikiano huo ni muhimu katika kuhakikisha miradi ya miundombinu inatekelezwa kwa kuzingatia mabadiliko na mwenendo wa hali ya hewa nchini.







Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Soma Taarifa ya UTEUZI:Rais Jakaya Kikwete amemteua Dkt. Ben E. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya PUMA Energy (zamani ilijulikana kama BP Ltd)

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

BINTI WA KITANZANIA GLORIA MAJULE ASHINDA TUZO YA UANDISHI BORA WA FILAMU YA MALARIA MAREKANI ‎

KOCHA WA MC ALGERS AIHOFIA YANGA

MAMBO 16 USIYOYAJUA KUHUSU RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE

VIONGOZI NA WATENDAJI WA MATAWI UVCCM PANGANI WANOLEWA

HIZI HAPA TAKWIMU ZA PETER SHALULILE MCHEZAJI MPYA WA YANGA SC 🔰 🔥