RAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na kumpangia kituo Balozi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi na kupangiwa kituo ni kama ifuatavyo:
(i) Dkt. Suleiman Peter Kiula ameteuliwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO). Dkt. Kiula anachukua nafasi ya Shaibu Ramadhan Matessa ambaye atapangiwa majukumu mengine;
(ii) Balozi Meja Jenerali Mbaraka Naziad Mkeremy amepangiwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia.


Comments