UWT KIBAHA MJI YAWAPIGA MSASA WA KUJIKWAMUA KIUCHUMI KWA WANAWAKE 400 WA KATA SABA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wawake (UWT) Wilaya ya Kibahaa mjini Elina Mgonja Katika kuuunga juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwakomboa wanawake kiuchumi  ameamua kutoa  mafunzo ya ujasiriamali  kwa vitendo  kwa  wanawake  wapatao  400 wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha  Mkoa wa Pwani  kwa lengo la  kuondokana na wimbi la umasikini.

Akizungumza   katika  ziara yake  maaalumu  ya kikazi yenye lengo la kuwatembelea wanawake wa (UWT) katika kata mbali mbali kwa ajili ya kuwapa maarifa na ujuzi na  kujifunza jinsi ya kutengeneza  bidhaa za aina tofauti ambazo zitawapa fursa ya kujiajiri  wao  wenyewe na kuondokana na kuwa tegemezi kila kukicha.

Elina amebainisha kuwa amefanya ziara hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake ambayo aliitoa ya kuwasaidia wanawake wa UWT kutoka kata zote 14 zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na kwamba mafunzo hayo ambayo ameamua kuyatoa bure bila malipo yoyote yatakuwa ni mkombozi mkubwa katika kujikwamua kiuchumi,
Nao baadhi ya wanawake ambao wamepata  mafunzo hayo  akiwemo Mwajuma Makuka  wamesema kwamba maffunnzo hayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na kuwa tegemezi na kwamba  watakwenda kuyafanyia kazi  kwa hali na mali kwa lengo la kuweza kuondokana na wimbi  la umasikini.

"Kwa kweli tunapenda kumshukuru kwa dhati Mwenyekiti wetu wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini Elina Mgonjwa kwa kuweza kufanya ziara hii na kuja kutupa elimu na mafunzo ya ujasiliamali na tumeweza kujifunza mambo mbali mbali ikiwemo kutengeneza bidhaa kama vile kutengeneza batiki, sabuni za kufulia, sabuni za kuogea pamoja na kupata ujuzi ambao tutakwenda kuufanyia kazi katika kutekeleza majukumu yetu,"amebainisha Mwajuma.
 
Mwenyekiti huyo  wa UWT anaendelea na ziara yake  ya kikazi ambapo hadi sasa ameshatembelea kata 7 ambazo ni Msangani, Mkuza, Tumbi, Maili moja, Kongowe, Kibaha pamoja na Kata ya Misususugu ambapo jumla ya wanawake 400 wameweza kunufaika na mafunzo hayo ya ujasiriamali kwa vitendo.
                                                      



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Soma Taarifa ya UTEUZI:Rais Jakaya Kikwete amemteua Dkt. Ben E. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya PUMA Energy (zamani ilijulikana kama BP Ltd)

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

BINTI WA KITANZANIA GLORIA MAJULE ASHINDA TUZO YA UANDISHI BORA WA FILAMU YA MALARIA MAREKANI ‎

KOCHA WA MC ALGERS AIHOFIA YANGA

VIONGOZI NA WATENDAJI WA MATAWI UVCCM PANGANI WANOLEWA

MAMBO 16 USIYOYAJUA KUHUSU RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE

HIZI HAPA TAKWIMU ZA PETER SHALULILE MCHEZAJI MPYA WA YANGA SC 🔰 🔥