VIKUNDI VYA CBRM VYATAKIWA KUWA WALINZI WA BARABARA ITILIMA ‎

 


NA MWANDISHI WETU, SIMIYU

‎VIKUNDI vya Kijamii vinavyotekeleza matengenezo ya kawaida ya barabara kupitia Mpango wa CBRM unaotekelezwa na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) vimetakiwa kushirikiana na wananchi katika kulinda na kutunza miundombinu ya barabara ili iweze kudumu na kuendelea kutoa huduma kwa jamii.

‎Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Anna Gidarya wakati wa mafunzo yaliyowakutanisha jumla ya vikundi 16 kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutekeleza kwa ufanisi shughuli za matengenezo madogo madogo ya barabara katika maeneo yao.

 Gidarya amesema barabara ni mali ya wananchi na ni sehemu muhimu ya kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii hivyo amewataka wanavikundi pamoja na wananchi kwa ujumla kuwa mstari wa mbele kuzilinda dhidi ya vitendo vinavyoweza kusababisha uharibifu wa miundombinu hiyo.

‎Aidha, amevipongeza vikundi hivyo kwa kupata fursa ya kushiriki moja kwa moja katika matengenezo ya barabara akieleza kuwa hatua hiyo si tu inasaidia kuboresha miundombinu bali pia inawapa wananchi nafasi ya kushiriki katika maendeleo ya maeneo yao.

‎ Gidarya pia amewataka wanavikundi kuwa na umoja, mshikamano na ushirikiano huku wakiepuka migogoro na changamoto za ndani zinazoweza kuathiri utekelezaji wa majukumu yao.

‎Kwa upande wao, washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru TARURA kwa kuwajengea uwezo kuhusu utekelezaji wa matengenezo ya kawaida ya barabara ambapo wameahidi kutumia maarifa waliyoyapata kuwa mabalozi wa utunzaji wa miundombinu pamoja na kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya vikundi vyao.

‎Wamesema watahakikisha manufaa yanayotokana na ushiriki wao katika mpango huo yanatumika kuchochea maendeleo ya mtu mmoja mmoja, vikundi na jamii kwa ujumla.






Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Soma Taarifa ya UTEUZI:Rais Jakaya Kikwete amemteua Dkt. Ben E. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya PUMA Energy (zamani ilijulikana kama BP Ltd)

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

VIONGOZI NA WATENDAJI WA MATAWI UVCCM PANGANI WANOLEWA

NMB YAWAUNGANISHA WANANCHI NA HUDUMA, FURSA ZANZIBAR

HIZI HAPA TAKWIMU ZA PETER SHALULILE MCHEZAJI MPYA WA YANGA SC 🔰 🔥

KAMATI YA BUNGE PAC YABAINI MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA UMMA MZUMBE