ZOEZI LA UVUTAJI NYAYA AWAMU YA PILI ENEO LA KIKOMBO NA MKONZE KATIKA MRADI WA CHALINZE–DODOMA KUANZA KESHO


NA MWANDISHI WETU

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limewakumbusha wananchi kuwa, kuanzia Agosti 11 hadi 17, 2026, mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Kusafirisha Umeme wa Msongo wa Kilovolti 400 Chalinze–Dodoma ataendelea na zoezi la uvutaji wa nyaya kwa awamu ya pili katika eneo la Kikombo na Mkonze, Dodoma, katika mradi huo ambao uko mbioni kukamilika.


Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Irene Gowelle, amesema hatua hiyo imekuja baada ya awamu ya kwanza ya uvutaji wa nyaya kutoka Chalinze hadi Mkambarani, Morogoro, kufanyika kwa mafanikio makubwa.


Amesema kutokana na kazi hiyo, baadhi ya mikoa itapata umeme kwa ratiba maalumu. Mikoa hiyo ni ile inayopatikana katika Kanda ya Kati, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Kusini Magharibi na Kanda ya Ziwa. Aidha, amesisitiza kuwa mikoa ambayo haitaathirika katika kanda hizo ni pamoja na Morogoro na Tanga.


Ameongeza kuwa mikoa inayotoka katika  Kanda hizo  zitakosa umeme kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni. Hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za kukamilisha mradi huo, ambao unatarajiwa kuwa na mchango chanya katika kuimarisha mfumo wa usafirishaji na upatikanaji wa umeme nchini.


‘’Hii ni awamu ya pili ya zoezi la uvutaji wa nyaya katika eneo la Kikombo na Mkonze Mkoani Dodoma, niwaondoe hofu wananchi kwamba tutaendelea kutoa ratiba za upatikanaji wa umeme kupitia mitandao yake ya kijamii, ili kuwawezesha wananchi kupanga shughuli zao kulingana na ratiba hiyo’’alisisitiza Gowelle.


Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa Kilovolti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma unatarajiwa kukamilika Agosti 21, 2026. Kukamilika kwake kutaongeza uwezo wa mfumo wa usafirishaji wa umeme nchini na kuimarisha upatikanaji wa huduma ya umeme yenye ubora na uhakika kwa wananchi.




Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Soma Taarifa ya UTEUZI:Rais Jakaya Kikwete amemteua Dkt. Ben E. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya PUMA Energy (zamani ilijulikana kama BP Ltd)

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

BINTI WA KITANZANIA GLORIA MAJULE ASHINDA TUZO YA UANDISHI BORA WA FILAMU YA MALARIA MAREKANI ‎

KOCHA WA MC ALGERS AIHOFIA YANGA

VIONGOZI NA WATENDAJI WA MATAWI UVCCM PANGANI WANOLEWA

MAMBO 16 USIYOYAJUA KUHUSU RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE

HIZI HAPA TAKWIMU ZA PETER SHALULILE MCHEZAJI MPYA WA YANGA SC 🔰 🔥