PROF. SHEMDOE AKUTANA NA VIONGOZI WA MBINGA KUIMARISHA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

 

NA OWM – TAMISEMI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe, amefanya kikao kazi na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, wabunge na viongozi wa Wilaya ya Mbinga, kwa lengo la kujadili namna bora ya kuimarisha na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Mbinga.


Kikao hicho kimejikita katika kujadili hatua na mikakati inayoweza kuchukuliwa ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Mbinga inasimamiwa na kutekelezwa kwa ufanisi, kwa kuzingatia mahitaji na maslahi ya wananchi.


Kikao kazi hicho kimefanyika Septemba 22, 2026, katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Magogoni ya Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini.








Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUAPISHWA NDEJEMBI KUWA MAKAMU WA RAIS

𝐌𝐉𝐔𝐄 𝐊𝐀𝐂𝐇𝐄𝐑𝐎 𝐌𝐙𝐄𝐍𝐀

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

URUSI, CHINA, IRANI NA KOREA KASKAZINI WAPANGA KUUNDA JESHI MOJA LA KUJIHAMI

KATIKA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA.

PANYA MAGAWA WA SUA TANZANIA AJENGEWA MNARA WA HESHIMA CAMBODIA