SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS KUFUATIA KIFO CHA MAMA FATMA KARUME

 

Ninaungana na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoa salamu za pole kwa Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Familia, Wananchi wa Zanzibar, Watanzania na Waombolezaji Wote kufuatia kifo cha Mama Fatma Karume, Mjane wa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na maombolezo, ninawaombea wafiwa wote faraja, subira na nguvu za kustahimili pengo kubwa lililoachwa na mpendwa wetu.

Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, amjalie pumziko la milele na awape moyo wa subira wote walioguswa na msiba huu mkubwa.

“Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.”

Deogratius Ndejembi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUAPISHWA NDEJEMBI KUWA MAKAMU WA RAIS

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

𝐌𝐉𝐔𝐄 𝐊𝐀𝐂𝐇𝐄𝐑𝐎 𝐌𝐙𝐄𝐍𝐀

URUSI, CHINA, IRANI NA KOREA KASKAZINI WAPANGA KUUNDA JESHI MOJA LA KUJIHAMI

KATIKA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA.

PANYA MAGAWA WA SUA TANZANIA AJENGEWA MNARA WA HESHIMA CAMBODIA