WAZIRI MHE. KAIRUKI AWASILI NEW YORK KUSHIRIKI UNGA81

  Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb.), amewasili jijini New York, Marekani, kushiriki katika Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81), pamoja na mikutano mbalimbali ya kimataifa inayofanyika pembezoni mwa mkutano huo.


Akiwa New York, Waziri Kairuki anashiriki katika Jukwaa la Siku ya Ushirikiano wa Kidijitali 2026 (Digital Cooperation Day 2026), lenye kaulimbiu “Shaping a Global AI Future Through Science, Policy, and Capacity.” Jukwaa hilo linawakutanisha viongozi wa Serikali, wadau wa teknolojia, wataalamu na washirika wa maendeleo kujadili namna ya kujenga mustakabali wa kidijitali na Akili Unde (AI) unaojumuisha na kunufaisha nchi zote.

Katika jukwaa hilo, Tanzania itashiriki katika meza ya majadiliano ya Mawaziri, itakayojikita katika hatua za kuimarisha ulinzi na usalama wa Miundombinu ya Umma ya Kidijitali (Digital Public Infrastructure – DPI), pamoja na mijadala kuhusu maendeleo na matumizi ya Akili Unde (Artificial Intelligence – AI) na teknolojia ya Tokenization.

Ushiriki wa Tanzania utatoa pia fursa ya kuwasilisha mwelekeo na mtazamo wa nchi kuhusu maendeleo, usimamizi na matumizi salama na yenye tija ya Akili Unde, hususan katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Aidha, Tanzania itatumia jukwaa hilo kuangazia fursa na changamoto zinazolikabili Bara la Afrika katika zama za AI, ikiwemo mahitaji ya miundombinu ya kidijitali, uwezo wa kompyuta kwa ajili ya AI (AI computing capacity), upatikanaji na matumizi salama ya data, ukuzaji wa ujuzi wa kidijitali na AI, pamoja na uwekezaji na rasilimali fedha zinazohitajika kuwezesha nchi za Afrika kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali duniani.

Ushiriki huo unalenga pia kuhimiza sauti na ushiriki wenye maana wa nchi za Afrika katika mijadala na maamuzi ya kimataifa kuhusu AI, hususan katika uundaji wa sera na mifumo ya usimamizi wa teknolojia hiyo, ujenzi wa uwezo wa kitaalamu, pamoja na uwekezaji katika miundombinu muhimu ya kidijitali.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUAPISHWA NDEJEMBI KUWA MAKAMU WA RAIS

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

𝐌𝐉𝐔𝐄 𝐊𝐀𝐂𝐇𝐄𝐑𝐎 𝐌𝐙𝐄𝐍𝐀

URUSI, CHINA, IRANI NA KOREA KASKAZINI WAPANGA KUUNDA JESHI MOJA LA KUJIHAMI

KATIKA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA.

PANYA MAGAWA WA SUA TANZANIA AJENGEWA MNARA WA HESHIMA CAMBODIA