WIZARA YA NISHATI YATWAA TUZO YA WIZARA BORA KWA UTENDAJI MEL 2026


NA MWANDISHI WETU, ARUSHA

WIZARA ya Nishati imeibuka kinara kwa kutwaa Tuzo ya Wizara Bora kwa Utendaji (Best Performing Ministry Award) katika eneo la Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza (MEL), katika Kongamano la Tano la Kitaifa la Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza (MEL 2026) linaloendelea jijini Arusha.


Tuzo hiyo imekabidhiwa tarehe 23 Septemba 2026 na Naibu Spika wa Bunge, Daniel Sillo (Mb), wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano la Tano la Kitaifa la Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza (MEL 2026). 


Tuzo hiyo inaitambua Wizara ya Nishati kwa utendaji na matumizi ya mifumo ya Ufuatiliaji na Tathmini katika kuimarisha utekelezaji wa mipango, programu na miradi ya Sekta ya Nishati.


Akizungumza kuhusu mafanikio hayo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Nishati, Anitha Ishengoma, amesema Wizara inajivunia kutambuliwa kwa juhudi na mafanikio yake katika eneo la Ufuatiliaji na Tathmini, jambo linalodhihirisha dhamira ya Wizara katika kuimarisha utendaji unaozingatia ushahidi na matokeo.


“Tunajivunia kuona juhudi na mafanikio ya Sekta ya Nishati katika Ufuatiliaji na Tathmini yakitambuliwa kwa kutunukiwa Tuzo ya Sekta Bora kwa Utendaji 2026. Tuzo hii ni matokeo ya kazi ya pamoja, uwajibikaji, ushirikiano na kujituma kwa Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zilizo chini yake,” amesema Ishengoma.


Amefafanua kuwa mafanikio hayo yanaakisi dhamira ya Wizara ya kuendelea kutumia Ufuatiliaji na Tathmini kama nyenzo muhimu ya kusimamia utendaji, utekelezaji wa mipango, programu na miradi, pamoja na kuwezesha ufanyaji wa maamuzi unaozingatia ushahidi na matokeo.


“Tunatoa shukrani kwa uongozi, watumishi na wadau wote waliochangia kufanikisha mafanikio haya. Tuzo hii si mwisho wa safari, bali ni chachu ya kuongeza kasi, ubora, uwajibikaji na kuleta matokeo yenye tija katika Sekta ya Nishati kwa manufaa ya wananchi,” amesisitiza Ishengoma







Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUAPISHWA NDEJEMBI KUWA MAKAMU WA RAIS

𝐌𝐉𝐔𝐄 𝐊𝐀𝐂𝐇𝐄𝐑𝐎 𝐌𝐙𝐄𝐍𝐀

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

URUSI, CHINA, IRANI NA KOREA KASKAZINI WAPANGA KUUNDA JESHI MOJA LA KUJIHAMI

KATIKA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA.

PANYA MAGAWA WA SUA TANZANIA AJENGEWA MNARA WA HESHIMA CAMBODIA