HAKUNA KUPOA, NGORONGORO YATOKA KIVINGINE



Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imezindua kituo maalum cha huduma kwa wateja kwa lengo la kuwahudumia wadau mbalimbali wa Uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii kwa karibu kinachojulikana Kama *Wateja Experience Centre.*


Akizindua kituo hicho Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro, Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Venance Mabeyo amepongeza menejimenti ya Ngorongoro kwa ubunifu na hatua ya uanzishwaji wa kituo hicho  ili kuboresha huduma kwa wateja, kutangaza mazao ya utalii na kuongeza uzoefu usiosahaulika kwa wateja wanaotembelea eneo la hifadhi ya Ngorongoro.


Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro Abdul-Razaq Badru ameeleza kuwa wateja watakaotembelea  kituo hicho elimu ya Vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro na gharama zake, huduma za vibali vya kwenda hifadhini, fursa za uwekezaji, kuunganisha wadau wa utalii na watalii wakiwa Ngorongoro, kupata mafunzo kwa waongoza utalii kuhusu mifumo ya malipo na vivutio vinavyopatikana,  kupokea maoni na mrejesho wa wadau kuhusu huduma wanazopata Ngorongoro.


Meneja Utalii na Masoko wa SACC, Mariam Kobelo, amesema kufunguliwa kwa kituo hicho ni sehemu ya mkakati wa shirika  kuboresha miundombinu na huduma za utalii ambapo Arusha kama kitovu cha utalii ofisi hiyo itakuwa One Stop Centre ya huduma zote za wageni, ikiwa ni maandalizi ya kupokea maelfu ya wageni wa AFCON 2027.


Kituo hicho kitatoa taarifa kuhusu maajabu yaliyopo Ngorongoro, huduma wanazohitaji kuzijua wateja na jinsi wateja wanavyoweza kuelezea mabadiliko ambayo wanahitaji kuyaona.




Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA

MWENGE WA UHURU WAMURIKA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KWELA

SERIKALI ITAENDEA KUHIMIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI- LONDO

NMB, UDSM waendeleza ushirikiano wa kukuza vipaji