NDEJEMBI ASHIRIKI IBADA YA MISA TAKATIFU YA KUMBUKIZI YA MIAKA 27 YA HAYATI NYERERE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi ameshiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya Miaka 27 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Epifania Jimbo Katoliki Sumbawanga, leo tarehe 14 Oktoba 2026.

 

Ibada hiyo, imeongozwa na Askofu Damian Kyaruzi wa Jimbo Katoliki Sumbawanga na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere, pamoja na Viongozi mbalimbali, waumini na wananchi mbalimbali.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akisalimiana na Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya Miaka 27 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Epifania Jimbo Katoliki Sumbawanga, leo Oktoba 14 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Baba wa Taifa Hayati. Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambao ni Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Makongoro Nyerere mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya Miaka 27 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Epifania Jimbo Katoliki Sumbawanga, leo Oktoba 14 2026.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba na Mkewe Mama Neema Nchemba, katika picha ya pamoja na Askofu Damian Kyaruzi, Mapadre pamoja na familia ya Baba wa Taifa Hayati. Mwl. Julius Kambarage Nyerere, mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya Miaka 27 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Epifania Jimbo Katoliki Sumbawanga, leo Oktoba 14 2026.

 

 



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA

MWENGE WA UHURU WAMURIKA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KWELA

KATIKA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA.

SERIKALI ITAENDEA KUHIMIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI- LONDO