Mbunge wa Jimbo la Nyang'wale, Hussein Amar ameitaka Serikali kutekeleza ahadi za marais kuhusu ujenzi kwa kiwango cha lami Barabara ya Kahama - Busisi.
Ametoa hoja hiyo wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni Dodoma Oktoba 28, 2026 na kujibiwa na Waziri wa Ujeni, Masanja Kadogosa.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Asha-Rose Migiro, amefungua semina elekezi kwa Kaimu Makatibu wa CCM Mikoa 32, leo Septemba 29, 2026, jijini Dodoma. Semina hiyo ya siku mbili inalenga kuwajengea uwezo viongozi hao kuhusu majukumu yao ya kiuongozi, uendeshaji wa shughuli za chama pamoja na utekelezaji wa mipango na maelekezo ya Chama Cha Mapinduzi. Akifungua semina hiyo, Ndugu Migiro amesisitiza umuhimu wa viongozi hao kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, weledi na kuzingatia misingi, kanuni na taratibu za chama.
Comments