MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI WILAYA YA TEMEKE NDUGU HAMISI SLIM AKIWA KATA ZA BUZA NA KILAKALA KATIKA ZOEZI LA USAJILI WA WANACHAMA WAPYA KATIKA MFUMO WA KIELEKTRONIKI.

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Temeke ametembelea kata ya Buza Mtaa wa mashine ya maji ikiwa ni sehemu ya kuhamadisha uandikishaji na usajili wa wanachama wapya wa CCM kwa mfumo wa kielektroniki.

Akiwa Buza mwenyekiti wa wazazi amelipa ada ya miaka mitatu kwa Mzee mmoja asiejiweza ikiwa kama sehemu ya kuhamasisha zoezi hilo na kumpatia Mzee uyo tabasamu la uanachama hai ndani ya chama cha mapinduzi.

Pia Ndugu Hamisi Slim amefika ktk kata ya Kilakala na kufanya hamasa kubwa katika zoezi la usajili wa wanachama wapya, huku akiwatia moyo wazee wa kijiwe cha wazee cha Bongotonyo, 

Akiwa kijiweni hapo mwenyekiti uyo wa wazazi Temeke amewataka wazee kuendelea kusimamia malezi na maadili ya vijana wetu wa Kilakala, huku akichangia uendeshaji wa kijiwe kwa kulipia bili ya king'amuzi cha Azam kijiweni hapo kwa miezi miwili mfululzo.


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MWENGE WA UHURU WAMURIKA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KWELA

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA

SERIKALI ITAENDEA KUHIMIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI- LONDO

NMB, UDSM waendeleza ushirikiano wa kukuza vipaji