NDEJEMBI AKUTANA NA RAIS MUSEVENI KUJADILI MAENDELEO YA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA EACOP

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), linalounganisha Hoima nchini Uganda na Chongoleani, Tanga nchini Tanzania.


Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ikulu ya Entebbe nchini Uganda, yakilenga kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati, hususan katika sekta ya mafuta na gesi.


Mkutano huo umehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe; Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Meja Jenerali Marco Gaguti; Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia mafuta na gesi, Dkt. James Mataragio; Kamishna wa Mafuta na Gesi, Goodluck Shirima, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mussa Makame.





Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MWENGE WA UHURU WAMURIKA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KWELA

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA

SERIKALI ITAENDEA KUHIMIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI- LONDO

NMB, UDSM waendeleza ushirikiano wa kukuza vipaji