NI MWENDO WA KUWAVURUGA WANYAMA PORI WAKALI NA WAHARIBIFU*


 NA MWANDISHI WETU 

Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la *Ngorongoro* (NCAA) tarehe 3 Novemba, 2026, imekabidhi Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kituo cha mwitikio wa haraka kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu kilichojengwa  katika Kijiji cha Naalarami, Wilaya ya Monduli, Mkoani Arusha.


Akizungumza wakati wa kukabidhi kituo hicho Naibu Kamishna wa Uhifadhi anayesimamia Huduma za Shirika Ngorongoro *Aidan Makala* amesema kuwa ujenzi wa vituo vya askari wa wanyamapori kwa ajili ya kutoa mwitikio wa haraka kwa matukio yanayohusisha wanyamapori wakali na waharibifu ni sehemu ya mchango wa Mamlaka katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kukabiliana na changamoto  hiyo.


Amesema lengo la Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia taasisi zake ni kuimarisha usalama wa wananchi, ambapo tayari *Ngorongoro imejenga vituo hivyo Monduli, Babati, Same, Korogwe na Rufiji.*


Msimamizi wa Ujenzi wa Kituo hicho *Mhandisi Faraja Sembua* ameeleza kuwa mradi wa ujenzi wa kituo hicho uliofanyika kwa kipindi cha miezi mitano na kugharimu shilingi milioni 102 ambapo kituo kinajumuisha ofisi, vyumba vya kulala, na sehemu za kuhifadhi silaha, choo na bafu pamoja na miundombinu mingine muhimu.


Akipokea kituo hicho Kamishna Msaidizi Mwandamizi kutoka *TAWA  P.M Kasisi* ametoa shukrani kwa *Ngorongoro* kuunga mkono juhudi za kudhibiti migangano ya wanyamapori wakali na waharibifu kwa mali za wananchi na kuahidi kusimamia  kituo hicho  ili kiwe na manufaa kwa wananchi .





Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MWENGE WA UHURU WAMURIKA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KWELA

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA

SERIKALI ITAENDEA KUHIMIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI- LONDO

NMB, UDSM waendeleza ushirikiano wa kukuza vipaji