TIMU YA NGORONGORO KAMA DOUMBIA


NA MWANDISHI WETU 

TIMU ya Mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro imeagwa leo Novemba 4, 2026 kuelekea mkoani Morogoro kushiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) ambapo imesafiri ikiwa na  ari ya kurudi na ushindi mnono kupitia michezo ya mpira wa Miguu, Netbali, Vollebal, Kamba na Michezo ya Jadi na Kuahidi kurudi na vikombe.


Akizungumza kwa niaba ya kamishna wa Uhifadhi wakati akiwaaga wachezaji hao, Naibu Kamishna huduma za Shirika, Aidan Makala , amewaasa washiriki kuzingatia nidhamu ya hali ya juu katika kipindi chote cha mashindano, akisisitiza kuwa nidhamu, umoja na ushirikiano ni msingi muhimu wa mafanikio katika michezo.


“Mnapoenda kushiriki michezo mnaitangaza Ngorongoro kupitia utalii wa michezo, ni mategeo yangu kuwa  mtakuwa mabalozi wa Ngorongoro, kuzingatia nidhamu, maadili na sheria za nchi na kuhakikisha kuwa timu yetu inarudi na vikombe vya kutosha”amesisitiza Makala

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MWENGE WA UHURU WAMURIKA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KWELA

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA

SERIKALI ITAENDEA KUHIMIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI- LONDO

NMB, UDSM waendeleza ushirikiano wa kukuza vipaji