TUKIKUBALI MIGAWANYIKO, NCHI HAITATAWALIKA – ASKOFU CHANDE

 ASKOFU Mkuu wa Makanisa ya Karmeli Assemblies of God Tanzania (KAG), Dkt. Evance Chande, amewataka Watanzania kukataa migawanyiko na kuwa makini dhidi ya watu wanaochochea mifarakano, akisisitiza kuwa kukubali hali hiyo kunaweza kuhatarisha umoja, amani na utulivu wa nchi.

Akizungumza Novemba 8, 2026, katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kanisa la KAG, eneo la Lugala, Nala jijini Dodoma, Askofu Chande alisema wananchi wana wajibu wa kulinda umoja wa taifa kwa kutoruhusu tofauti mbalimbali kutumiwa kuwagawanya.

Alisisitiza kuwa kila mmoja anapaswa kuwa sehemu ya kuimarisha mshikamano badala ya kuunga mkono vitendo vinavyoweza kuleta mifarakano katika jamii.

Kupitia harambee hiyo, jumla ya Sh milioni sita zilichangwa papo kwa papo, huku washiriki wengine wakitoa ahadi za kuchangia fedha kwa ajili ya kufanikisha hatua hiyo ya ujenzi.

Ujenzi wa kanisa hilo kubwa umefikia hatua ya linta, hatua inayotangulia kuendelea na kazi nyingine za ujenzi kuelekea kukamilika kwa jengo hilo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini kutoka madhehebu tofauti, waliotoka ndani ya Dodoma na mikoa mingine, ikiwa ni sehemu ya kushiriki tukio hilo la uwekaji wa jiwe la msingi.

Askofu Mkuu wa KAG, Dkt. Evance Chande akifunua pazia ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kanisa hilo.

Jengo la Kanisa ambalo ujenzi wake unaendelea.
Askofu Mkuu wa KAG, Dkt. Chande akilakiwa alipowasili katika sherehe hizo.



Kwaya ya watoto ikitumbuiza.
Baadhi ya waumini na wageni waalikwa wakiwa katika sherehe hizo.


Askofu Mkuu Chande akihubiri.
Mchungaji wa kanisa hilo jipya, Mtema Chinyele akijitambulisha pamoja na mkewe Imelda.
Baadhi ya viongozi wa dini walioalikwa.

Katibu Mkuu wa KAG akiratibu sherehe hizo.







Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MWENGE WA UHURU WAMURIKA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KWELA

NMB, UDSM waendeleza ushirikiano wa kukuza vipaji

SERIKALI ITAENDEA KUHIMIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI- LONDO

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA